Thursday, 24 May 2018

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye Kipindi cha Siku Mpya kinachurushwa na Redio Boma Hai 89.3 FM.  (Picha na Adrian Lyapembile)

Korosho kuimarisha Uchumi Wilaya ya Hai



Katibu Tawala Wilaya ya HAi Upendo Wella (aliyevaa miwani na skafu nyeusi) akiwaongoza viongozi wa ngazi mbalimbali kulipokea zao la korosho na kuinua juu miche ya zao hilo kama ishara ya kuinua uchumi katika Wilaya ya Hai (Picha zote na Praygod Munisi)


Watanzania Watakiwa Kuiunga Mkono Serikali

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hasani Abbas (Mwenye miwani kulia) akisisitiza jambo alopofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Halmashuri pamoja na kufahamu changamoto wanazokutana nazo. (Picha na Adrian Lyapembile)

Saturday, 28 April 2018

Hai yapanda miti kusheherekea miaka 54 ya Muungano



Katibu Tawala Wilaya ya Hai Bi. Upendo Wella akiongoza zoezi la upandaji miti katika kijiji cha Mtakuja kata ya Kia.

Kameshina wa scout Mkoa wa Kilimanjaro Broity Maktora akishiriki zoezi la upandaji miti.

Afisa maliasili Wilaya ya Hai Bw. Mbayan Mollel akishiriki zoezi la upandaji miti kusheherekea miaka 54 ya muungano.

''Wazazi Wapelekeni Watoto Kupata Chanjo''DC HAI

Mkuu wawilaya ya Hai Mh. Onesmo Buswelu wakati akizindua chanjo ya polio kwa watoto katika Hospital ya Wilaya ya Hai

Thursday, 26 April 2018

HAI ya sheherekea Muungano kwakupanda miti

Na Zaina Andrew na Praygod Munis

HAI

Wakati maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyo fanyika leo mjini Dodoma, halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamesherehekea sikukuu hiyo  kwa kupanda miti katika kata ya Kia kijiji cha Mtakuja.

Katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wella amesema kutokana na watu kushidwa kwenda kwenye maadhimisho hayo mjini Dodoma hivyo ameona ni vyema kutumia muda huo  kwa ajili yakupanda miti ili kuboresha mazingira ya wilaya ya Hai pia taifa kwa ujumla, sambamba na kauli mbiu ya "TANZANIA YAKIJANI INAWEZEKANA  PANDA MITI KWA MAENDELEIOYA VIWANDA" .

Naye kamishina  wa scout mkoani Kilimanjaro Broity Maktora amesema kuwa wameadhimisha muungano kwa kupanda miti kwa lengo la kuboresha amani ya Taifa la Tanzania pia   kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa  kuifanya Kilimanjaro kuwa ya kijani.

Hata hivyo afisa maliasili wa wilaya ya Hai Mbayani Moleli ameeleza kuwa kutakana na changamoto nyingi zinazowakabili zaidi kwenye utunzaji wa miti hiyo kwa baadhi ya wafugaji ila ameeleza kuwa wametoa elimu kwa wanajamii na pia wataendelea kutoa elimu hiyo ili kuweza kuimarisha na kuboresha utunzaji wa miti hiyo .

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja  Teheraki Kipara Moleli amezungumza kuwa kutokana na elimu iliyotolewa kwa wamajamii  wamekuwa na uelewa wa umuhimu wa kupanda miti kwani wanajamii hao  wanajitihada kubwa ya kuzidi kupanda miti kwenye makazi yao hivyo  wanatarajia mabadiliko makubwa ya uboreshwaji wa  mazingira.

Saturday, 21 April 2018

DC ahimiza shughuli za kimaendeleo





Mkuu wa Wilaya Ya Hai Mh. Onesmo Buswelu katikati akisikilza maelezo kutoka kwa kamati ya shule ya sekondary Longoi iliyopo kata ya  weru weru wilayani Hai mara baada yakufika shuleni hapo.


Kamati ya shule ya Sekondary Longoi wakimsikiliza kwa umakini mkuu wawilaya ya Hai Onesmo Buswelu baada yakutembelea shuleni hapo.

DC HAI AAGIZA MTO KUFANYIWA USAFI BAADA YA MAFURIKO KUTOKEA



Meneja wa TARURA Wilaya ya Hai Mhandisi Charles Marwa (kulia) akitoa maelezo katika kijiji cha sanya station katika kata ya Kia baada yakukumbwa na mafuriko.

Mkuu wa wilaya ya Hai Mh. Onesmo Buswelu Akitoa maelekezo kwa viongozi wa kijiji cha sanya station, pamoja na maafisa mazingira wilaya mara baada ya kijiji hicho kukumbwa na mafuriko.

Mkazi wa kijiji cha sanya station akizungumzia athari ziliz
otokea mara baada ya mafuriko kutokea kijijini hapo.




Eneo ambalo mto umeacha njia yake rasmi nakutengeneza mto mwingine pembeni mara baada ya mvua kubwa kunyesha katika kijiji cha sanya station kata ya Kia wilayani Hai( Picha zote na Davis Minjer)


Wednesday, 11 April 2018

TASAF yazidi kuwanufaisha kaya masikini Hai


Na Omary Mlekwa

HAI

WANUFAIKA wa mpango wa kunusuru kaya maskini unaondeshwa na mfuko wa jamii (TASAF) wameshauriwa  kutumia fedha wanazopata kuanzisha shughuli za ujasiriamali ili kuondokana na hali tegemezi .

Wananchi Watakiwa Kutunza Miti Wanayootesha

Na Omary Mlekwa Hai


MKUU wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Onesmo Buswelu amewataka wananchi kutunza miti inayooteshwa katika kipindi hiki cha mvua ili iweze kukua na kukabiliana na hali ya ukame kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Friday, 9 March 2018

WANAWAKE WASHAURIWA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI ILI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA




 Na Edwine Lamtey

HAI.

Wanawake wametakiwa kujituma na kujiamini katika shughuli mbali mbali za kiuchumia hapa nchini ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali kwa njia ya kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kujikimu katika maisha ya sasa  pamoja na kufikia uchumi wa viwanda .

UKOSEFU WA SOKO LA UHAKIKA WA BIDHAA ZA NGOZI WAPELEKEA WAFANYA BIASHARA KUOMBA KUUZA BIDHAA HIYO NJE YA NCHI





Na Salma Shabani

SIHA,

Wafanayabiasha wa bidhaa za Ngozi Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro,wameomba Serikali kuwaruhusu kuuza bidha hiyo nje ya nchi kutokana na kukosa soko la uhakika hapa nchini

Wednesday, 7 March 2018

SERIKALI KILIMANJARO YASHAURIWA KUTOA ELIMU KWA WAVUVI



 

Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Mkoa Wa Kilimanjaro mwalimu Mgala Ramadhani [katikati} wakati akizungumza na waandishi wa Habari Kilimanjaro.[picha na Edwine Lamtey]


CCM HAI YACHANGIA VIFAA VYA UJENZI KWAAJILI YA UKARABATI WA SHULE




HAI 
CHAMA cha mapinduzi (CCM) Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kimetoa msaada wa vifaa vya ujenzi katika shule ya msingi Kibohehe kwa lengo la kukarabati shule hiyo ambayo iliezuliwa paa na kuharibika miundombinu yake na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja wa darasa la Sita 

Tuesday, 6 March 2018

Madereva bodaboda chanzo cha ujauzito kwa wanafunzi wilayani Hai.

Na Zaina Andrea na Agness  Mchome
HAI
Madereva wa Boda boda wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro  wamebainika kuwa ndilo kundi linalosababisha kuwapa ujauzito  wanafunzi hasa wale wa sekondari wilayani Hai.

Sunday, 4 March 2018

MOTO WATEKETEZA VIBANDA VYA WAFANYA BIASHARA HAI

Na Latifa Botto
HAI
Zaidi ya vibanda saba vinavyotumika kama maduka katika eneo la Machine tools wilayani Hai mkoani Kilimanjaro vimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo huku wafanyabiashara wa eneo hilo wakidai kupata hasara kubwa.

Wazazi waaswa kutowatelekeza watoto wao Mashuleni

Na Davis Minja
HAI
Wazazi na Walezi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuacha tabia ya kuwatelekeza watoto katika shule wanazo soma pasipo kuwa nao karibu, hali inayosababisha  watoto kukosa upendo na malezi kutoka kwa wazazi.

MOTO WATEKETEZA VIBANDA VYA WAFANYA BIASHARA HAI

Na Latifa Botto
HAI

Zaidi ya vibanda saba vinavyotumika kama maduka katika eneo la Machine tools wilayani Hai mkoani Kilimanjaro vimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo huku wafanyabiashara wa eneo hilo wakidai kupata hasara kubwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Isa amesema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme uliosababisha vibanda saba kuteketea kwa moto.

Kwa upande wake mwenyekiti  wa kijiji cha wari ndoo ambaye pia ni shuhuda wa ajali hiyo ya moto bwana Emanuel muro wakati akizungumza na redio boma hai fm eneo la tukio wilayani hai amethibitisha pia kutokea kwa moto huo huku akidai hali halisi ya hasara iliyopatikana bado haijafahamika hadi sasa.

Ameongeza kwa kusema kuwa serikali iwafikirie wafanyabiashara waliopata hasara ya kuunguliwa na maduka yao pamoja na hilo serkali inapaswa kuwapa kibali cha kujenga majengo na si vibanda na kuboresha miundombinu haswa ya maji.

Kwa upande wa mmoja wa wamiliki wamaduka yaliyoungua Bw. Stanley Mushi amesema kuwa moto huo uliosababishwa na hitilafu ya umeme na kuliomba shirika la umeme  kuangalia suala hilo na kurekebisha miundombinu yake

Thursday, 1 March 2018

Polisi Yaimarisha ulinzi shuleni baada ya wanafunzi kufanya vurugu

Na Omary Mlekwa 

JESHI la polisi mkoa wa Kilimanjaro,limeimarisha  ulinzi na usalama katika shule ya sekondari ya Lyamungo iliyopo kata ya Machame Mashariki wilayani Hai kufuatia vurugu zilizojitokeza baina ya wanafunzi na walimu wa nidhamu wa shule hiyo.

Vurugu za wanafunzi zasababisha shule kufungwa kwa muda Hai

NA OMARY MLEKWA

HAI
 
SERIKALI wilaya Hai mkoani Kilimanjaro imeifunga shule ya Sekondari ya Lyamungo kwa zaidi ya wiki mbili baada ya Wanafunzi kufanya vurugu na uharibifu wakipinga mwenzao kufukuzwa shuleni hapo.

Monday, 26 February 2018

UKAME UNAOENDELEA WAKWAMISHA MAENDELEO YA MITI WILAYA YA HAI



NA Agness Mchome
Hai

Wafanyakazi na watunzaji wa miti katika kitengo cha Green Tree Nurcery  eneo la boma wilayani Hai wamelalamika juu ya  ukame unaoendelea kuwa ni changamoto kubwa inayo sababisha maendeleo ya miti kikwama .

Wakizungumza na Boma hai fm wafanyakazi hao ambao ni Joyce Michael na  Abel Kweka wamezungumzia changamoto hiyo na kusema baadhi ya miti kwa sasa imekauka kwa kukosa maji hali inayopelekea wao kukosa baadhi ya mahitaji yao kwani wameajiriwa na wanategemea mshahara kutoka  katika kitengo hicho.

Kwa upande wake meneja wa kitengo hicho Baraka kweka  amesema kuwa kwa sasa hali ni ngumu kutokana na bili za maji kuongezeka hali inayosababisha miti hiyo kukosa maji mengi  na kushindwa kuuzika hivyo kupunguza wafanyakazi  ili kuepuka hasara.

Meneja huyo ameeleza kuwa kuna baadhi ya changamoto zingine ambazo ni pembejeo kama vile viriba kwa ajili ya kutunzia miti pamoja na pampu za maji ambapo amesema kuwa ni chache na zinapelekea uzalishaji kuwa mdogo na kipato kushuka.

Aidha Baraka ameiomba serkali kupunguza angalau bili za maji ili kufanya miti hiyo kupata maji kwa urahisi na kufanya biashara hiyo kukua zaidi na kufikia sehemu  ya kipato kikubwa.

HALI NGUMU YA BIASHARA YAZIDI KUTIKISA WAFANYA BIASHARA WILAYANI HAI



NA mwandishi; ZAINA ANDREA




HAI

Wafanyabiashara wadogo wadogo katika eneo la stendi ya Sanya juu wilayani hai wanapambana na hali ngumu ya biashara kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali masokoni.

Akizungumza na radio boma fm mjasiriamali na mfanya biashara Jesca James, amesema kuwa kwa sasa wanafanya biashara kwa lengo la kulinda mtaji kutokana na hali ngumu ya biashara na wala sikwaajili ya kupata faida.

Amesema kupanda kwa bei ya Nyanya, vitunguu,matunda pamoja na usafirishaji wa bidhaa hizo pia ni changamoto kwao kwani wanafanyakazi bila ya kipato kinachowaridhisha katika kazi zao.

Aidha wamesema pamoja na hayo wanaendelea vizuri katika kutunza mazingira ya maeneo hayo kwa kutii sheria na taratibu zilizowekwa na serikali ya mamlaka ya mji mdogo wa Bomang’ombe.

Pia  Wameiomba serikali iwasaidie kwa kuwawezesha katika biashara zao ili kuendelea kijikimu kimaisha kupitia biashara zao za kila siku.

Saturday, 24 February 2018

Hai yatoa taarifa ya mapato na matumizi 2017/2018

Na Omary Mlekwa
HAI

HALMASHAURI ya wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, imetumia zaidi ya shilingi bil  13  ambayo ni sawa na asilimia 34  ya makisio ya bajeti ya mwaka 2017/2018 ya mapato na matumizi ya  shilingi bil  38.

Shule Yafungwa Kwa Muda Usiojulikana

Na Omary Mlekwa
Hai

Serikali Mkoani Kilimanjaro imeifunga shule ya msingi Kibohehe iliyopo wilaya ya Hai kwa mda usijulikana ili kupisha ukarabati wa shule hiyo  kutokana na baadhi ya miundombinu yake  kuharibiwa vibaya na mvua na upepo .

Tuesday, 20 February 2018

Watakiwa Kuutunza Mlima Kilimanjaro





Afisa maliasili Wilaya ya Hai Bw.Mbayani Mollel akitoa mafunzo juu ya mazingira kwa waalimu wa mazingira kutoka shule 25 wilayani Hai. (picha zote na praygod Munisi)






Mtaalamu wakilimo Wilaya ya Hai Bw.Simon Gunda akitoa maelezo wakati wa warsha ya mafunzo ya uhifadhi mlima Kilimanjaro kwa waalimu wamazingira kutoka shule 25 wilayani Hai.


Afisa mazingira wilaya ya Hai Bw.Njigite akitoa maelezo wakati wa warsha ya mafunzo ya uhifadhi mlima Kilimanjaro kwa waalimu wamazingira kutoka shule 25 wilayani Hai.




Baadhi ya Waalimu kutoka katika shule 25 walayani Hai wakifuatilia kwa makini mafunzo ambayo yanahusu utunzaji wa mazingira yaliyo tolewa katika warsha ya siku moja na wataalam wanaohusika na mazingira.


Na Praygod Munisi na Davis Minja
HAI

Imeelizwa kuwa jamii ya watu wanao ishi karibu na Hifadhi ya mlima Kilimanjaro,wana wajibu mkubwa wakusaidia kutunza Mlima kilimanjaro ili kuendelea kupata faida na huduma zitokanazo na Mlima huo.

Hayo yamebainishwa leo na Afisa mali asili wa Wilaya ya Hai Mbayani Mollel wakati wa warsha ya mafunzo ya siku moja ya uhifadhi wa mlima kilimanjaro kwa waalimu wa mazingira toka shule 25 za msingi pamoja na waratibu elimu kata.

Amesema kuwa kwa sasa bado kuna uhitaji mkubwa kwa jamii zilizo zunguka mlima huo kuweka nguvu kwa kushirikiana na klabu za mazingira zilizopo shuleni ili kuweka msisitizo kwa wanafunzi kuwa na chachu ya kuhifadhi mazingira.

Mollel ameongeza kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazo kabili uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na,uvamizi wa misitu kwaajili ya kilimo,kuchoma misitu,kuingiza mifugo katika hifadhi ya misitu pamoja na ukataji miti kiholela jambo ambalo limekuwa likitishia hali ya uhifadhi wa mazingira.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi wa warsha hiyo Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Hai Edward Mtakiliho amepongeza jitihada zinazo endelea kufanywa na walimu wa mazingira katika shule 25 zinazo zunguka mlima huo ambazo zimeonesha jitihada chanya za barafu ya mlima kilimanjaro kuongezeka au kubakia katika hali ya matumaini ya kuongezeka.

Ameongeza kuwa ikiwa jamii yote pasipo kutegemea uhifadhi huo kufanywa na wanafunzi au shule hali ya mazingira inaweza kuboreshwa kwa kiasi kikubwa na kuzidi kuleta mafanikio zaidi.

Naye Rais wa Rotary klabu ya machame Raymond Uronu ameitaka serikali kuongeza nguvu katika makali ya sheria zinazo tumika kusimamia mazingira ili sheria hizo ziweze kufanya kazi kama ilivyo kusudiwa.

Uharibifu wa misitu Tanzania kwa mwaka ni Hekta 372,000  ambapo ni uvunaji haramu, moto, uvamizi mipaka,huku Mahitaji ya ujazo wa miti ni M3 milioni 62.3 na kilichopo ni M3 milioni 42.8 hivyo upungufu ni M3 milioni 19.5 kwa ajili ya matumizi Upungufu huu wa mahitaji ni kichocheo cha uvunaji haramu wa misitu na kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji na upotevu wa misitu na ongezeko la hewa ukaa.


Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...