HAI
CHAMA cha mapinduzi (CCM)
Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kimetoa msaada wa vifaa vya ujenzi katika shule
ya msingi Kibohehe kwa lengo la
kukarabati shule hiyo ambayo iliezuliwa paa na kuharibika miundombinu yake na
kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja wa darasa la Sita
Hatua ya CCM ya kuwapatia vifaa hivyo vya ujenzi ili
kuharakisha ukarabati wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi waweze kurejea
shuleni hapo ambapo kwa sasa wamehamishiwa katika shule za jirani
Akizungumza na wajumbe wa
serikali ya kijiji pamoja na wataalamu wakati akikabidhi msaaada huo Mwenyekiti
wa CCM, Wilaya ya Hai, Wang’uba Magai amesema chama cha mapinduzi kitakuwa bega
kwa bega kuhakikisha wanatoa msaada pale
utakapohitajika ikiwa ni pamoja na kufuatilia
shughuli nzima ya ujenzi shuleni hapo.
Msaada uliotolewa shuleni
hapo ni pamoja na mifuko 37 ya sementi,
misumari kilo 10 pamoja na chokaa ambapo ujenzi huo utaanza na vyumba sita vya madarasa .
Kwa upande wake mkuu wa
Wilaya ya Hai mshikizi mhe, Onesmo Buswelu ameunga mkono jitihada za mwenyekiti wa CCM
kwa kuongeza mifuko 10 ya sementi na matofali elfu moja kwa lengo la kusaidia
ujenzi huo kwenda haraka ili wanafunzi
waweze kurejea shuleni hapo.
Nae mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Hai, Yohana Sintoo amesema kwenye
fedha za miradi ya maendeleo wameweka
kiasi cha shilingi milioni moja na hamsini
ambapo fedha hizo zikipatikana
zitasaidia ukarabati wa madarasa hayo kukamilika haraka kabla ya mwezi wa sita na wanafunzi kurejea.
Shule ya msingi Kibohehe
,ilipata maafa baada ya Ukuta wake kuanguka Mnamo Februari 22 mwaka huu na
kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja huku wengine watatu wakijeruhiwa na
serikali kuamuru kufungwa kwa muda kupisha ukarabati
No comments:
Post a Comment