Saturday, 21 April 2018

DC ahimiza shughuli za kimaendeleo





Mkuu wa Wilaya Ya Hai Mh. Onesmo Buswelu katikati akisikilza maelezo kutoka kwa kamati ya shule ya sekondary Longoi iliyopo kata ya  weru weru wilayani Hai mara baada yakufika shuleni hapo.


Kamati ya shule ya Sekondary Longoi wakimsikiliza kwa umakini mkuu wawilaya ya Hai Onesmo Buswelu baada yakutembelea shuleni hapo.



Na Davis Minjer_ Hai

WANANCHI  Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kushiriki na kuhimiza shughuli za maendeleo katika maeneo yao,hasa katika sekta ya elimu ili kuandaa kizazi cha wasomi wa kusaidia Taifa na siyo kufuata kila linalo semwa na wanasiasa wanaopinga maendeleo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Onesmo Buswelu wakati akizungumza na kamati ya shule ya sekondari Longoi iliyopo kata ya weruweru kwaajili ya kufufua jitihada za kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kupunguza adha wanazo pata wanafunzi na waalimu wakati wa kutimiza majukumu yao.

Kwa upande wake Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Jasper Mbwambo amebainisha changamoto zilizopo katika shule hiyo ikiwemo upungufu wa madarasa tisa hali inayo pelekea wanafunzi 80 kutumia chumba kimoja hali inayo leta usumbufu.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya Shule hiyo Suleman mvungi amebainisha kuwa kusuasua kwa shughuli ya maendeleo katika kata hiyo ni kutokana na wananchi kuingiza siasa kwa kila maamuzi ya kufikia maendeleo jambo linalo kwamisha hata vikao vyao ndani ya kijiji.

Shule ya Sekondari longoi ina wanafunzi 852 ikiwemo wanafunzi 245 kidato cha kwanza,377 kidato cha pili,126 kidato cha tatu na 104 kidato cha nne jambo linalo pelekea kuwa na ukosefu wa vyumba vya madarasa tisa kutokana na sasa kuwa na vyumba vya madarasa 12 tu.

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...