NA Agness Mchome
Hai
Wafanyakazi
na watunzaji wa miti katika kitengo cha Green Tree Nurcery eneo la boma wilayani Hai wamelalamika juu
ya ukame unaoendelea kuwa ni changamoto
kubwa inayo sababisha maendeleo ya miti kikwama .
Wakizungumza
na Boma hai fm wafanyakazi hao ambao ni Joyce Michael na Abel Kweka wamezungumzia changamoto hiyo na
kusema baadhi ya miti kwa sasa imekauka kwa kukosa maji hali inayopelekea wao
kukosa baadhi ya mahitaji yao kwani wameajiriwa na wanategemea mshahara
kutoka katika kitengo hicho.
Kwa upande
wake meneja wa kitengo hicho Baraka kweka
amesema kuwa kwa sasa hali ni ngumu kutokana na bili za maji kuongezeka
hali inayosababisha miti hiyo kukosa maji mengi
na kushindwa kuuzika hivyo kupunguza wafanyakazi ili kuepuka hasara.
Meneja huyo
ameeleza kuwa kuna baadhi ya changamoto zingine ambazo ni pembejeo kama vile
viriba kwa ajili ya kutunzia miti pamoja na pampu za maji ambapo amesema kuwa
ni chache na zinapelekea uzalishaji kuwa mdogo na kipato kushuka.
Aidha Baraka
ameiomba serkali kupunguza angalau bili za maji ili kufanya miti hiyo kupata
maji kwa urahisi na kufanya biashara hiyo kukua zaidi na kufikia sehemu ya kipato kikubwa.