Sunday, 4 March 2018

MOTO WATEKETEZA VIBANDA VYA WAFANYA BIASHARA HAI

Na Latifa Botto
HAI

Zaidi ya vibanda saba vinavyotumika kama maduka katika eneo la Machine tools wilayani Hai mkoani Kilimanjaro vimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo huku wafanyabiashara wa eneo hilo wakidai kupata hasara kubwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Isa amesema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme uliosababisha vibanda saba kuteketea kwa moto.

Kwa upande wake mwenyekiti  wa kijiji cha wari ndoo ambaye pia ni shuhuda wa ajali hiyo ya moto bwana Emanuel muro wakati akizungumza na redio boma hai fm eneo la tukio wilayani hai amethibitisha pia kutokea kwa moto huo huku akidai hali halisi ya hasara iliyopatikana bado haijafahamika hadi sasa.

Ameongeza kwa kusema kuwa serikali iwafikirie wafanyabiashara waliopata hasara ya kuunguliwa na maduka yao pamoja na hilo serkali inapaswa kuwapa kibali cha kujenga majengo na si vibanda na kuboresha miundombinu haswa ya maji.

Kwa upande wa mmoja wa wamiliki wamaduka yaliyoungua Bw. Stanley Mushi amesema kuwa moto huo uliosababishwa na hitilafu ya umeme na kuliomba shirika la umeme  kuangalia suala hilo na kurekebisha miundombinu yake

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...