Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Mkoa Wa Kilimanjaro mwalimu Mgala Ramadhani [katikati} wakati akizungumza na waandishi wa Habari Kilimanjaro.[picha na Edwine Lamtey] |
Na Edwine Lamtey
MOSHI
Serikali imeshauriwa kutafuta njia
mbadala ikiwemo ya utoaji wa elimu na ukamataji wa wavuvi haramu katika kulinda
rasilimali zilizopo ndani ya bwawa la Nyumba ya Mungu badala ya kulifunga
ambapo hali hiyo imedaiwa kuathiri wananchi wanaotegemea shughuli za uvuvi
katika bwawa hilo.
Akitoa rai hiyo mwenyekiti wa chama
cha ACT wazalendo mkoa wa Kilimanjaro mwalimu Mgala Ramadhani amesema kuwa
badala ya serikali kuwekeza nguvu kubwa katika kukamata na kufanya msako wa
samaki katika soko la Manyema ni vyema serikali ikaweka mkakati wa kuwachukulia
hatua wanaotumia zana zisizo stahili katika bwawa hilo pamoja na kutoa elimu kwa
wananchi juu ya njia sahihi ya kufanya uvuvi.
Kauli hiyo ya ACT inakuja baada ya
agizo la mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bi Anna mghwira kulifunga bwawa la Nyumba
ya mungu kwa kile kilichoelezwa kuwa samaki wanaovuliwa ni wadogo kupita kiasi
na hivyo kuamua kulifunga bwawa hilo.
Kwa upande wake katibu wa chama hicho
Ally Mdimu amesema kuwa badala ya nguvu kubwa kutumika kuwasaka wanaoingiza
samaki katika soko la manyema ni vyema nguvu hiyo ikaelekezwa katika kulinda
bwawa hilo kwani hata samaki hao wanapokamatwa katika soko hilo ni dhahiri kuwa
uharibifu umekwishafanyika na haiwezekani kuwarudisha tena katika bwawa hilo.
Sanjari na hayo katibu huyo
amepongeza juhudi zinazofanya na serikali na kusema kuwa chama cha ACT
wazalendo kitazidi kuunga mkono jitihada nzuri katika kuheshimu misingi ya
utawala bora huku kikipinga siasa za majungu na wasiopenda maendeleo.
No comments:
Post a Comment