Na Salma Shabani
SIHA,
Wafanayabiasha wa
bidhaa za Ngozi Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro,wameomba
Serikali kuwaruhusu kuuza bidha hiyo nje ya nchi kutokana na kukosa soko
la uhakika hapa nchini
Wakizungumza na
waandishi wa habari kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao
waamesema kuwa tangu kuwekwa kwa masharti ya kusafirisha bidhaa hiyo nje ya
nchini wamekuwa wakipata hasara kutokana na kukosa soko la uhakika hapa nchini
Mmoja wa wafanyabiashara
hao ,Zakaria Materu amesema kuwa tangu mwaka 2015 kumekuwepo mlundikano wa
ngozi nyingi hali ambayo imesababisha kuendelea kuishi maisha magumu
Amesema serikali
wakati ikiwakwenye mchakato wa ufufuaji wa vyema vya ngozi hapa nchini ni vyema
wakawaruhusu kuendelea na kuuza ngozi nchi ya nchi ili kunusuru wafanyabiashara
hao kupata hasara
Alisema kabla ya zuio
la Serikali wafanyabiashara kutoka Nchini Kenye walikuwa wakinunua kwa
shilingi 8000 hadi 5000 ngozi moja lakini kwa sasa hakuna anayeuliza bei
Nae mfanyabiashara e
Lasteck Gideon,alisema wakati serikali ikijipanga kuingia kwenye uchumi wa
viwanda ingewaruhusu kuuza ngozi hizo ili kulinda mitaji yao,sambamba na
kuiongezea serikali mapato
Afisa mifugo wa Wilaya
hiyo Barnabas Mbwambo,alisema kuwa Ngozi zipo nyingi sana kwenye wilaya yake,
sina idadi ya tani lakini ni nyingi hata Wilaya za jirani tunamawasiliano nao
wanadaia ngozi ni nyingi na kwamba hakuna soko
No comments:
Post a Comment