Na Omary Mlekwa
JESHI la polisi mkoa wa Kilimanjaro,limeimarisha ulinzi na usalama katika shule ya sekondari ya Lyamungo iliyopo kata ya Machame Mashariki wilayani Hai kufuatia vurugu zilizojitokeza baina ya wanafunzi na walimu wa nidhamu wa shule hiyo.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake mjini Moshi ,mkoani Kilimanjaro, kamanda Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah,alisema kwamba jeshi hilo imeendelea kuimarisha ulinzi.
Kamanda alisema wanafunzi hao zaidi ya 444 wa kidato cha tano na sita walivamia nyumba ya walimu wa Nidhamu Safari Rasin Mwasile(32) na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyumba hiyo pamoja na kuharibu migomba iliyopo shambani.
“Tukio hilo limetokea Februali 28 mwaka huu majira ya saa nne asabuhi wanafunzi zaidi ya 444 walivamia nyumba ya walimu huyo wa nidhamu na kuvunja milango vyioo vya nyumba hiyo na kung’oa bati ,pia walivamia shamba la migomba na kukatakata migomba yote,”alisema Kamanda Issah.
“Wanafunzi hao walikuwa wakituhumu walimu huyo kuwa tukana matusi ya nguoni,jeshi tunaendelea kuchunguza chanzo cha uharibifu huo, kwamba tukio hilo haliwezi kuvumbiwa macho ,”alisema.
Hata hivyo Chanzo cha mgogoro huo unadaiwa kuwa ulitokana na uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ya shule ,ambapo inadaiwa katika upigaji kura mmoja mwanafunzi aliandika matusi kwenye karatasi ya kura,ambapo baada
Inasemekana kwamba baada utambuzi wa hati mwanafunzi aliyeandika matusi ,hati alibainika na mwanafunzi huyo alipewa adhabu ya kurudishwa nyumbani ndipo wanafunzi wenzake waligoma kuingia darasani huko wakidai kwamba mwalimu wa nidhamu ndiye chanzo cha matusi hayo.
No comments:
Post a Comment