Thursday, 25 January 2018

TUJIKUMBUSHE KIDOGO KUHUSU MAZINGIRA

Na Praygod Munisi

Hifadhi ya mazingira ni juhudi zinazofanywa na binadamu ili kuhakikisha ulimwenguanamoishi usiharibiwe na utendaji wake, bali uweze kuwafaa watu wa vizazi vijavyo.

Tunatakiwa tutunze mazingira kwani tukiyachafua tutapata magonjwa ya mlipukokama vile kipindupindu na mengine mengi.

Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka sisi wanadamu. Kwa mfano: miti, mito, maziwa, nyumba n.k. Mazingira yanafaa kuwekwa safi wakati wote kwani yana faida kubwa katika maisha ya mwanadamu ingawaje katika duniahii ya sasa watu wamekuwa wakiharibu mazingiryanayowazunguka. Mfano: watu wanakata miti ovyo, wanachafua vyanzo vya maji; uchafuzi huo unapelekea hata wanyamakukimbia makazi yao na kwenda kutafuta makazi mengine.

Pia kutokana na ukataji miti ovyo imepelekea ukosefu wa mvua, na hii imepelekea kuanguka kwa kilimo duniani na kusababisha njaa katika baadhi ya maeneo, hasa katika nchi za Asia.

Pia joto kuongezeka: kwa mfano huko Indiajoto lilipanda juu sana hivyo kupelekea vifo.

Kwa hayo machache tunaona athari za uchafuzi wa mazingira; ni vyema tukajitahidi kuyatunza mazingira yetu ili kuweza kupata manufaa kutoka kwenye mazingira yetu wenyewe.

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...