Thursday, 26 April 2018

HAI ya sheherekea Muungano kwakupanda miti

Na Zaina Andrew na Praygod Munis

HAI

Wakati maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyo fanyika leo mjini Dodoma, halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamesherehekea sikukuu hiyo  kwa kupanda miti katika kata ya Kia kijiji cha Mtakuja.

Katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wella amesema kutokana na watu kushidwa kwenda kwenye maadhimisho hayo mjini Dodoma hivyo ameona ni vyema kutumia muda huo  kwa ajili yakupanda miti ili kuboresha mazingira ya wilaya ya Hai pia taifa kwa ujumla, sambamba na kauli mbiu ya "TANZANIA YAKIJANI INAWEZEKANA  PANDA MITI KWA MAENDELEIOYA VIWANDA" .

Naye kamishina  wa scout mkoani Kilimanjaro Broity Maktora amesema kuwa wameadhimisha muungano kwa kupanda miti kwa lengo la kuboresha amani ya Taifa la Tanzania pia   kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa  kuifanya Kilimanjaro kuwa ya kijani.

Hata hivyo afisa maliasili wa wilaya ya Hai Mbayani Moleli ameeleza kuwa kutakana na changamoto nyingi zinazowakabili zaidi kwenye utunzaji wa miti hiyo kwa baadhi ya wafugaji ila ameeleza kuwa wametoa elimu kwa wanajamii na pia wataendelea kutoa elimu hiyo ili kuweza kuimarisha na kuboresha utunzaji wa miti hiyo .

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja  Teheraki Kipara Moleli amezungumza kuwa kutokana na elimu iliyotolewa kwa wamajamii  wamekuwa na uelewa wa umuhimu wa kupanda miti kwani wanajamii hao  wanajitihada kubwa ya kuzidi kupanda miti kwenye makazi yao hivyo  wanatarajia mabadiliko makubwa ya uboreshwaji wa  mazingira.

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...