NA OMARY MLEKWA
HAI
SERIKALI wilaya Hai mkoani Kilimanjaro imeifunga shule ya Sekondari ya Lyamungo kwa zaidi ya wiki mbili baada ya Wanafunzi kufanya vurugu na uharibifu wakipinga mwenzao kufukuzwa shuleni hapo.
Hatua hiyo inatokana na uharibifu mkubwa uliofanywa na wanafunzi hao kwa kuharibu miundombinu ya shule hiyo ikiwemo nyumba ya mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo.
Mkuu wa wilaya hiyo mshikizi Onesmo Buswelu alisema hatua ya kuifunga shule hiyo ni ili kuepusha uharibu zaidi pamoja na uvunjifu wa amani.
"Kamati ya ulinzi na usalama imeridhia wanafunzi wote kuondoka shuleni na kwenda kwa wazazi wao na wanapaswa kurejea shuleni Machi 18 mwaka huu"aliseama
" Wanafunzi walifanya vurugu na fujo na hatimaye maandamo siku ya Feb 28 kwa lengo la kumwona mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya kuyokana na mwanafunzi mwenzao kuadhibiwa na mwalimu wa Nidhamu wa shule hiyo Safari Lasini "alisema
" Maandamo hayo yalikwamia katika eneo la Mashine Tools ambapo walikutana na Kaimu mkutugenzi wa Halmashauri ,Edward Ntakilio na wanafunzi walitii na kurejea shuleni "alisema
" Mwanafunzi wa kidato cha tano ,Moses Siima anayesoma mchepuo wa HGE,anadaiwa kuwatukana waalimu jambo ambalo lilisababisha kuadhibiwa pamoja na kusimamishwa masomo"alisema
Akitoa maamuzi hayo kwa wanafunzi hao Machi moja mwaka huu,kaimu mkurugenzi Ntakilio alisema wanafunzi watarejea shuleni hapo Machi 18 mwaka huu na endapo mwanafunzi atakosa kuripoti atahesabiwa kuwa mtoro.
"Maamuzi haya ni ya awali itaundwa kamati kwa ajili ya ufuatiliaji na kufanya tathimini ya uharibifu huo ili hatua zaidi za kisheria" alisema
No comments:
Post a Comment