NA
mwandishi; ZAINA ANDREA
HAI
Wafanyabiashara
wadogo wadogo katika eneo la stendi ya Sanya juu wilayani hai wanapambana na
hali ngumu ya biashara kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali
masokoni.
Akizungumza
na radio boma fm mjasiriamali na mfanya biashara Jesca James, amesema kuwa kwa
sasa wanafanya biashara kwa lengo la kulinda mtaji kutokana na hali ngumu ya
biashara na wala sikwaajili ya kupata faida.
Amesema
kupanda kwa bei ya Nyanya, vitunguu,matunda pamoja na usafirishaji wa bidhaa
hizo pia ni changamoto kwao kwani wanafanyakazi bila ya kipato
kinachowaridhisha katika kazi zao.
Aidha
wamesema pamoja na hayo wanaendelea vizuri katika kutunza mazingira ya maeneo
hayo kwa kutii sheria na taratibu zilizowekwa na serikali ya mamlaka ya mji
mdogo wa Bomang’ombe.
Pia
Wameiomba serikali iwasaidie kwa
kuwawezesha katika biashara zao ili kuendelea kijikimu kimaisha kupitia
biashara zao za kila siku.
No comments:
Post a Comment