Monday, 26 February 2018

UKAME UNAOENDELEA WAKWAMISHA MAENDELEO YA MITI WILAYA YA HAI



NA Agness Mchome
Hai

Wafanyakazi na watunzaji wa miti katika kitengo cha Green Tree Nurcery  eneo la boma wilayani Hai wamelalamika juu ya  ukame unaoendelea kuwa ni changamoto kubwa inayo sababisha maendeleo ya miti kikwama .

Wakizungumza na Boma hai fm wafanyakazi hao ambao ni Joyce Michael na  Abel Kweka wamezungumzia changamoto hiyo na kusema baadhi ya miti kwa sasa imekauka kwa kukosa maji hali inayopelekea wao kukosa baadhi ya mahitaji yao kwani wameajiriwa na wanategemea mshahara kutoka  katika kitengo hicho.

Kwa upande wake meneja wa kitengo hicho Baraka kweka  amesema kuwa kwa sasa hali ni ngumu kutokana na bili za maji kuongezeka hali inayosababisha miti hiyo kukosa maji mengi  na kushindwa kuuzika hivyo kupunguza wafanyakazi  ili kuepuka hasara.

Meneja huyo ameeleza kuwa kuna baadhi ya changamoto zingine ambazo ni pembejeo kama vile viriba kwa ajili ya kutunzia miti pamoja na pampu za maji ambapo amesema kuwa ni chache na zinapelekea uzalishaji kuwa mdogo na kipato kushuka.

Aidha Baraka ameiomba serkali kupunguza angalau bili za maji ili kufanya miti hiyo kupata maji kwa urahisi na kufanya biashara hiyo kukua zaidi na kufikia sehemu  ya kipato kikubwa.

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...