MOSHI
Idara ya Mifugo na
Uvuvi katika halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro,
imefanikiwa kuwaua mbwa wenye kichaa 96 kutoka katika kijiji cha Mawala,
Mikocheni, Msekia na Mtakuja.
Akizungumza katika
mahojiano maalum na mwandishi wa habari ofisini kwake afisa Mifugo na uvuvi Dkt
Walter Marandu, alisema kuwa halmashauri imechukua hatua za haraka za kuwaua
mbwa hao lengo likiwa ni kuwadhibiti wasiendelee kuleta madhara kwa binadamu.
Alisema kuwa tatizo la
uwepo wa ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni mkubwa, wapo mbwa wengi wenye ugonjwa
huo na takwimu tulizonazo kuanzia kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu watu
waliong’atwa na mbwa wafikia 64.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa halmashauri ya Moshi, Marco Kilawila alisema kuwa tayari
halmashauri hiyo imeshaanza zoezi la kuwachanja mbwa wote.
Hata hivyo aliwataka
wamiliki wote wa mbwa kuhakikisha kuwa wanapatiwa chanjo
zinazositahili kuanzia chanjo ya kichaa cha mbwa, pamoja na magonjwa mengine
ili kuepusha watu wasiendelee kupata madhara zaidi.
No comments:
Post a Comment