Sunday, 4 March 2018

Wazazi waaswa kutowatelekeza watoto wao Mashuleni

Na Davis Minja
HAI
Wazazi na Walezi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuacha tabia ya kuwatelekeza watoto katika shule wanazo soma pasipo kuwa nao karibu, hali inayosababisha  watoto kukosa upendo na malezi kutoka kwa wazazi.


Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai mshikizi Onesmo Buswelu wakati akikabidhi mifuko 75 ya saruji iliyo kuwa imeahidiwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira katika ujezi wa Bweni la Wanafunzi wa Shule ya St.Fransis Wa Sisi.

Kwaupande wake Mwalimu mkuu wa Shule hiyo Sister Costantine Mosha amekiri kuwepo kwa baadhi ya wazazi na walezi wanao kimbia majukumu ya kuwalea watoto wao na badala yake wanatumia fursa ya elimu kuwatelekezea wanafunzi shuleni huku wengine wakibadili namba za simu kuepuka kufuatiliwa.

WAKATI HUO HUO
Jeshi la polisi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro limeweka mikakati kuhakikisha  linadhibiti  vitendo vya utoaji mimba kwa wanafunzi  kwani ni hatari kwa maisha yao na jamii kwa ujumla.

Akizungumza na Redio Boma FM Mwenyekiti wa dawati  la jinsia wilayani Hai Happy Eliufoo amesema kwa sasa wameanza  kutoa elimu katika shule mbalimbali wilaya ya Hai kwa lengo la kudhibiti vitendo hivyo kwani ni kinyume cha sheria.

Kwa upande wao walimu katika shule ya Sekondari Hai wamesema wameanza kudhibiti suala hilo kwa kuchukua hatua ya kuwapima  ujauzito wanafunzi  ambapo suala hilo hufanyika kwa kila mwaka kwa awamu mbili.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa pindi wanapopata mimba hulazimika kutoa ili waweze kuendelea na elimu kutokana na agizo la Rais Dr.Magufuli kuwa mwanafunzi wa kike atakapopata ujauzito atalazimika kukatisha masomo yake haraka iwezekanavyo licha ya kufahamu kwamba kufanya hivyo  ni hatari kwa maisha yao.

Aidha baadhi ya wazazi  wamezungumzia suala hili na kusema kuwa ni hatari na hakuna mzazi anayefurahi mwanaye kufanya vitendo hivyo ambavyo pia ni kinyume na sheria za dini

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...