Na Salma Shabani
HAI
Wananchi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa
kuchukua taadhari ya kujikinga na ugonjwa wa kichaa cha Mbwa ulioripotiwa kuua
watu watatu wilaya ya moshi vijijini.
Akizungumza na redio boma hai fm Mganga mkuu wa
Hospitali ya wilaya ya hai Daktari Irine Haule amesema kuwa kila mwananchi
anapaswa kuchukua taadhari hiyo pamoja na watoto wadogo kuwa karibu na familia
zao kwa ulinzi zaidi.
Ameongeza kuwa kila mwananchi anapaswa kuchukua
taadhari za kufika katika vituo vya afya pindi wanapo ng’atwa na mbwa wanao
zurura hovyo na kuwataka waripoti katika vituo vya afya ili waweze kupatiwa
tiba.
Haule amewataka wamiliki wa mbwa kuwachanja mbwa wao wanao wafuga ili kuondokana na
ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na wamiliki wa mbwa hao kuwafungia ndani kipindi
cha mchana kwa taadhari zaidi kwani mbwa
kuzurura hovyo ni kuhatarisha maisha ya watu jambo ambalo ni kosa kisheria.
Ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni moja ya magonjwa
yanayo athiri maeneo mengi duniani,maradhi yanayo sababishwa na virusi kutoka
kwa wanyama jamii ya mbwa walio athirika na virusi hivyo,wakiwemo,fisi,paka na
mbweha.
Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 30-50 ya waathirika wa ugonjwa wa kichaa cha
mbwa ni watoto wenye umri chini ya miaka 15.
No comments:
Post a Comment