Rais Dkt. John Magufuli ametuma
salamu za rambirambi kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahimu Juma kufuatia
kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mh. Robert Kisanga kilichotokea
tarehe 23, Januari mwaka huu.
Katika salamu hizo Dkt. Magufuli
amesema Jaji Mstaafu Robert Kisanga atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa
alioutoa kwa taifa wakati wote wa utumishi wake uliojaa umakini, uchapakazi,
uzalendo na ushirikiano na wengine.
Mh Raisi amewaombea wafiwa wote wawe na moyo wa
subira,uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na
amemuombea marehemu Jaji mstaafu Kisanga apumzishwe mahali pema peponi, amina.