Afisa maliasili Wilaya ya Hai Bw.Mbayani Mollel akitoa mafunzo juu ya mazingira kwa waalimu wa mazingira kutoka shule 25 wilayani Hai. (picha zote na praygod Munisi) |
Mtaalamu wakilimo Wilaya ya Hai Bw.Simon Gunda akitoa maelezo wakati wa warsha ya mafunzo ya uhifadhi mlima Kilimanjaro kwa waalimu wamazingira kutoka shule 25 wilayani Hai. |
Afisa mazingira wilaya ya Hai Bw.Njigite akitoa maelezo wakati wa warsha ya mafunzo ya uhifadhi mlima Kilimanjaro kwa waalimu wamazingira kutoka shule 25 wilayani Hai. |
Na Praygod Munisi na Davis Minja
HAI
Imeelizwa kuwa jamii ya watu wanao
ishi karibu na Hifadhi ya mlima Kilimanjaro,wana wajibu mkubwa wakusaidia
kutunza Mlima kilimanjaro ili kuendelea kupata faida na huduma zitokanazo na
Mlima huo.
Hayo yamebainishwa leo na Afisa
mali asili wa Wilaya ya Hai Mbayani Mollel wakati wa warsha ya mafunzo ya siku
moja ya uhifadhi wa mlima kilimanjaro kwa waalimu wa mazingira toka shule 25 za
msingi pamoja na waratibu elimu kata.
Amesema kuwa kwa sasa bado kuna
uhitaji mkubwa kwa jamii zilizo zunguka mlima huo kuweka nguvu kwa kushirikiana
na klabu za mazingira zilizopo shuleni ili kuweka msisitizo kwa wanafunzi kuwa
na chachu ya kuhifadhi mazingira.
Mollel ameongeza kuwa zipo
changamoto mbalimbali zinazo kabili uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja
na,uvamizi wa misitu kwaajili ya kilimo,kuchoma misitu,kuingiza mifugo katika
hifadhi ya misitu pamoja na ukataji miti kiholela jambo ambalo limekuwa
likitishia hali ya uhifadhi wa mazingira.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika
uzinduzi wa warsha hiyo Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Hai Edward
Mtakiliho amepongeza jitihada zinazo endelea kufanywa na walimu wa mazingira
katika shule 25 zinazo zunguka mlima huo ambazo zimeonesha jitihada chanya za
barafu ya mlima kilimanjaro kuongezeka au kubakia katika hali ya matumaini ya
kuongezeka.
Ameongeza kuwa ikiwa jamii yote
pasipo kutegemea uhifadhi huo kufanywa na wanafunzi au shule hali ya mazingira
inaweza kuboreshwa kwa kiasi kikubwa na kuzidi kuleta mafanikio zaidi.
Naye Rais wa Rotary klabu ya
machame Raymond Uronu ameitaka serikali kuongeza nguvu katika makali ya sheria
zinazo tumika kusimamia mazingira ili sheria hizo ziweze kufanya kazi kama
ilivyo kusudiwa.
Uharibifu
wa misitu Tanzania kwa mwaka ni Hekta 372,000 ambapo ni uvunaji haramu, moto, uvamizi
mipaka,huku Mahitaji ya ujazo wa miti ni M3 milioni 62.3 na
kilichopo ni M3 milioni 42.8 hivyo upungufu ni M3 milioni
19.5 kwa ajili ya matumizi Upungufu huu wa mahitaji ni kichocheo cha uvunaji
haramu wa misitu na kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji na upotevu wa
misitu na ongezeko la hewa ukaa.
No comments:
Post a Comment