Inspector Shabo wa kituo cha polisi Bomang'ombe wakati akizungumza katika kikao cha mamlaka ya mji mdogo wa Hai |
Mwenyekiti wa mtaa wa Kingereka B, Saidi Seifu Mkambala wakati akizungumza katika kikao cha kamati ya mamlaka ya Mji mdogo wa Hai |
HAI
Viongozi wa serikali za mitaa wilayani Hai mkoani
Kilimanjaro wametakiwa kusimamia ulinzi na usalama katika mitaa yao na
kuhakikisha linaimarika hasa katika kipindi hiki cha mwishoni mwa mwaka.
Hayo yamesemwa na inspekta Shabo wa kituo cha polisi
Bomang’ombe wakati wakufanyika kwakikao cha kamati ya mamlaka ya mji mdogo wa
Hai,nakusisitiza kuwa viongozi hao wakiwa kama walinzi wa Amani katika mitaa,
hivyo ni vyema kuhakikisha usalma na mali za Wananchi zinakuwa salama muda wote
nakuhakikisha wanatokomeza kabisa vitendo vya ualifu katika mitaa yao
kwakushirikiana na jeshi la polisi.
Shabo amesisitiza kuwa
viongozi wa serikali za mitaa ni vyema wakatumia vikundi vya ulinzi shirikishi
vilivyopo katika mitaa yao ili vishirikiane na jeshi la polisi katika kupambana
na kupunguza uhalifu kwenye mitaa nakuwakumbusha wananchi umuhimu wakutumia
hivi vikundi.
‘’tuwakumbushe watu wetu hivi
vikundi ambavyo tulivyonavyo vifanye kazi ili tuweze kupunguza ualifu ambao
unaendelea kutokea’’alisema shabo.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa mtaa wa kingereka B katika mji wa Bomang’ombe Bw.Saidi Seifu
Mkambala amelishauri jeshi la polisi wilayani Hai kuzidi kuimarisha doria
katika mitaa hususa nikatika mji wa bomang’ombe kutokana nakuongezeka kwa
vitendo vya kiualifu nakuwaomba viongozi wenzake wa serikali za mitaa kutoa
ushirikiano wakutosha kwa jeshi hilo ili suala la ulinzi na usalama lizidi
kuimarika.
No comments:
Post a Comment