Saturday, 28 April 2018

Hai yapanda miti kusheherekea miaka 54 ya Muungano



Katibu Tawala Wilaya ya Hai Bi. Upendo Wella akiongoza zoezi la upandaji miti katika kijiji cha Mtakuja kata ya Kia.

Kameshina wa scout Mkoa wa Kilimanjaro Broity Maktora akishiriki zoezi la upandaji miti.

Afisa maliasili Wilaya ya Hai Bw. Mbayan Mollel akishiriki zoezi la upandaji miti kusheherekea miaka 54 ya muungano.



Na  Praygod Munisi Hai


Wakati maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyo fanyika  mjini Dodoma, halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamesherehekea sikukuu hiyo kwa kupanda miti katika kata ya Kia kijiji cha Mtakuja.

Katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wella amesema kutokana na watu kushidwa kwenda kwenye maadhimisho hayo mjini Dodoma hivyo ameona ni vyema kutumia muda huo kwa ajili yakupanda miti ili kuboresha mazingira ya wilaya ya Hai pia taifa kwa ujumla, sambamba na kauli mbiu ya "TANZANIA YAKIJANI INAWEZEKANA PANDA MITI KWA MAENDELEIOYA VIWANDA" .

Naye kamishina wa scout mkoani Kilimanjaro Broity Maktora amesema kuwa wameadhimisha muungano kwa kupanda miti kwa lengo la kuboresha amani ya Taifa la Tanzania pia kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa kuifanya Kilimanjaro kuwa ya kijani.

Hata hivyo afisa maliasili wa wilaya ya Hai Mbayani Moleli ameeleza kuwa kutakana na changamoto nyingi zinazowakabili zaidi kwenye utunzaji wa miti hiyo kwa baadhi ya wafugaji ila ameeleza kuwa wametoa elimu kwa wanajamii na pia wataendelea kutoa elimu hiyo ili kuweza kuimarisha na kuboresha utunzaji wa miti hiyo .

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja Teheraki Kipara Moleli amezungumza kuwa kutokana na elimu iliyotolewa kwa wamajamii wamekuwa na uelewa wa umuhimu wa kupanda miti kwani wanajamii hao wanajitihada kubwa ya kuzidi kupanda miti kwenye makazi yao hivyo wanatarajia mabadiliko makubwa ya uboreshwaji wa mazingira.

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...