Na Zaina Andrea na Agness Mchome
HAI
Madereva wa Boda boda wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamebainika kuwa ndilo kundi linalosababisha kuwapa ujauzito wanafunzi hasa wale wa sekondari wilayani Hai.
Hayo yamebainishwa na afisa wa Jeshi la polisi kitengo cha dawati jinsia Wilayani Hai koplo John Maziku wakati akizungumza na Redio Boma Hai fm na kusema kuwa kundi la Madereva wa Bodaboda na Bajaji ndio wanaohusika na suala la kuwapa ujauzito wanafunzi hasa wale wa shule za sekondari.
Kwa upande wao baadhi ya madereva wa Bodaboda wilayani Hai wamesema kuwa baadhi ya wanafunzi wakati mwingine wanashindwa kujitambua kwa kutojua ni nini wajibu wao hasa katika suala la kuzingatia masomo yao.
Wakizungumzia suala hili nao wanafunzi wameeleza kuwa mambo hayo hufanyika kwani wanafunzi wengine wanaishi mbali na makazi yao hivyo huamua kuchukua bodaboda na ndipo wanapowarubuni na kujihusisha na suala la kimapenzi na hatimaye kuapata ujauzito
No comments:
Post a Comment