Na Edwine Lamtey
HAI.
Wanawake wametakiwa kujituma na
kujiamini katika shughuli mbali mbali za kiuchumia hapa nchini ikiwa ni pamoja
na uzalishaji mali kwa njia ya kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili
kuweza kujikimu katika maisha ya sasa
pamoja na kufikia uchumi wa viwanda .
Hayo yamesemwa mapema hii leo na katibu
tawala wilaya ya Hai Bi Upendo Wella
wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kata ya masama
rundugai wilayani hai mkoani Kilimanjaro na kushirikisha wanawake mbali mbali
kutoka maeneo ya wilaya ya Hai.
Upendo Amesema ni vyema wanawake
wakajiunga katika vikundi mbali mbali vya ujasiriamalikwa lengo la kuanzisha viwanda vidodogo vidogo kwa kutumia
fursa za mikopo ya wanawake na vijana zinazotolewa na Halmashauri
Kwa upande wa wadau mbali mbali
waliohudhuria maadhimisho hayo, mwenyekiti wa dawati la Jinsia na watoto
wilayani Hai Coplo Happness Eliufoo amesema kuwa kwa sasa wanawake wanapaswa
kuzidi kusimama na kuendana na kasi ya kuelekea uchumi wa viwanda badala ya
kusubiri kuinuliwa kama ilivyokuwa hapo awali.
Naye mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la
voice of empowered women foundation bi lightness kimaro amesema kutokana na
kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na wanawake katika jamii shirika lao
limeweza kuwasaidia wanawake mbalimbali ambao wanakutana na changamoto ambazo
zinawakabili pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa wanawake.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya
maendeleo ya jamii Bwana lukasi msele amesema kuwa idara yamaendeleo ya jamii
wilaya ya Hai bado inazidi kuhamasisha na kutoa elimu juu ya kujiunga na
vikundi mbali mbali pamoja na kuwaelekeza njia sahihi ya kutumia fursa hizo za
mikopo ambapo wilaya ya Hai imekwishatoa mikopo hiyo kwa zaidi ya vikundi
vitano vya wanawake.
Kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka huu ni :kuelekea
uchumi wa viwanda tuimarishe uchumi wa jinsia na uwezeshaji wanawake vijijini.
No comments:
Post a Comment