Na Omary Mlekwa
HAI
WANUFAIKA wa mpango wa kunusuru kaya maskini unaondeshwa na
mfuko wa jamii (TASAF) wameshauriwa
kutumia fedha wanazopata kuanzisha shughuli za ujasiriamali ili
kuondokana na hali tegemezi .
Ushauri huo umetolewa na Bi
Sophia Gao mkazi mtaa wa Kia wilayani Hai mkoani Kilimanajro wakati
akielezea mafanikio aliyoyapata kutokana na fedha anazozipata kupitia TASAF,
jinsi zilivyoweza kubadilisha maisha yake.
Bi Gao amesema endapo
wanufaika na mpango huo wataweza kutumia fedha hizo kwa malengo zitawasadia
kuboresha hali ya maisha yao kuondokana
na hali tegemezi pindi mradi huo unapofikia mwisho.
Amesema kuwa anaishukuru
serikali kwa kumwezesha kubadilisha maisha yake ambapo awali alikuwa
akiishi maisha ya tabu kutokana na
kutokuwa na uwezo wa kuendesha maisha na
familia lakini kwa sasa maisha yake
yamebadilika kabisa.
Aidha Bi Gao amefafanua kuwa fedha alizopata tangu kuanzishwa
kwa mpango ameweza kuanzisha mgawaha pamoja na kibanda cha kuuzia matunda na
mboga mboga jambo ambalo limemsaidia
kuendesha familia yake pamoja na kuweza kununua eneo kwa ajili ya kujenga
nyumba ya kuishi.
Naye Bi Grace Macha ambaye
pia ni mnufaika amesema fedha alizopata kwa awamu 17 kutoka TASAF
ameweza kuanzisha ufugaji wa kuku pamoja na mbuzi hali iliyosaidia kuboresha
maisha yake ambapo hapo awali alikuwa akiishi kwa mlo mmoja lakini kwa sasa ana
uwezo wa kula mara tatu kwa siku.
Kwa upande wake, mratibu wa TASAF wilaya ya Hai , Bwana Erick Marishamu amesema tangu zoezi
hilo lianzishwe jumla ya shilingi bilioni 2.5 zimetumika kunufaisha
kaya 3905 katika vijiji 43 vilivyoko kwenye mpango huo.
No comments:
Post a Comment