Na Omary Mlekwa
Hai
Hai
Serikali Mkoani Kilimanjaro imeifunga shule ya msingi Kibohehe iliyopo wilaya ya Hai kwa mda usijulikana ili kupisha ukarabati wa shule hiyo kutokana na baadhi ya miundombinu yake kuharibiwa vibaya na mvua na upepo .
Mkuu wa Mkoa huo,Anna Mghwira alitoa agizo hilo baada ya kutembelea shule hiyo kujionea uharibifu uliotekea hali ambayo ilisababisha mwanafunzi mmoja wa dasasa la sita kupoteza maisha huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya.
Alisema uamuzi huo unatokana na kubaini kuwa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo umejengwa chini ya kiwango jambo ambalo lisipoangaliwa kwa umakini linaweza kusababisha madhara wengine kwa wanafunzi na watumishi wa shule hiyo.
"Tunafunga shule hii ili kupisha ukaratabi wa majengo na wanafunzi kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba watatawanywa katika shule nyingine za jirani mpaka pale ukarabati utakapokamilika" alisema Mghwira
"Wataalamu wa Halmashauri watafanya tathmini ya ukarabati na kutueleza mda halisi lakini pia ukarabati huo ,utakuwa na malengo wawili ya mda mrefu na mfupi ili wanafunzi warejee na kuendelea na masomo yao." alisisitiza
"Licha ya kufunga shule pia ujenzi wa shule hiyo ,ulijengwa chini ya kiwango na bila kufuata utaratibu za ujenzi agizo kukamatwa kwa msimamizi wa ujenzi pamoja na aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule kipindi ujenzi ulipofanyika" aliongeza
"Chanzo kikuu cha kuezuliwa kwa bati la chumba cha darasa la tatu ni kutokana na kujengwa chini ya kiwango na kukosekana kwa umakini pindi ujenzi ulipofanyika"
"Majengo haya yamejengwa chini ya kiwango na hayakufuata kanuni za ujenzi tena hayajafungwa lenta hali ambayo imesababisha kubomoka kwa utahisi " alisema Mghwira
Kwa upande wake mhandisi wa Halmashauri hiyo, Loshiwa Moleli alisema kuwa shule hiyo ilijengwa zamani na tayari walishashauri kuwa majengo hayo yavunjwe ili kuepuka madhara
"Mheshimiwa tayari tulishakagua majengo yamejengwa chini ya kiwango na tulishauri yajengwe mapya " alisema Moleli
Nae Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Aileni Lema alisema changamoto kubwa ni upungufu wa madarasa ambapo mpaka sasa wanavyumba sita vya madarasa ambavyo vinatumiwa na wanafunzi wa darasa la awali mpaka darasa la saba.
"Shule yetu ina wanafunzi 162 na haina vyumba vya madarasa ya awali na darasa la kwanza jambo linapelekea tutumie hata haya madarasa ambayo yamejengwa chini ya kiwango" alisema
No comments:
Post a Comment