Friday, 9 March 2018

WANAWAKE WASHAURIWA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI ILI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA




 Na Edwine Lamtey

HAI.

Wanawake wametakiwa kujituma na kujiamini katika shughuli mbali mbali za kiuchumia hapa nchini ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali kwa njia ya kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kujikimu katika maisha ya sasa  pamoja na kufikia uchumi wa viwanda .

UKOSEFU WA SOKO LA UHAKIKA WA BIDHAA ZA NGOZI WAPELEKEA WAFANYA BIASHARA KUOMBA KUUZA BIDHAA HIYO NJE YA NCHI





Na Salma Shabani

SIHA,

Wafanayabiasha wa bidhaa za Ngozi Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro,wameomba Serikali kuwaruhusu kuuza bidha hiyo nje ya nchi kutokana na kukosa soko la uhakika hapa nchini

Wednesday, 7 March 2018

SERIKALI KILIMANJARO YASHAURIWA KUTOA ELIMU KWA WAVUVI



 

Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Mkoa Wa Kilimanjaro mwalimu Mgala Ramadhani [katikati} wakati akizungumza na waandishi wa Habari Kilimanjaro.[picha na Edwine Lamtey]


CCM HAI YACHANGIA VIFAA VYA UJENZI KWAAJILI YA UKARABATI WA SHULE




HAI 
CHAMA cha mapinduzi (CCM) Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kimetoa msaada wa vifaa vya ujenzi katika shule ya msingi Kibohehe kwa lengo la kukarabati shule hiyo ambayo iliezuliwa paa na kuharibika miundombinu yake na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja wa darasa la Sita 

Tuesday, 6 March 2018

Madereva bodaboda chanzo cha ujauzito kwa wanafunzi wilayani Hai.

Na Zaina Andrea na Agness  Mchome
HAI
Madereva wa Boda boda wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro  wamebainika kuwa ndilo kundi linalosababisha kuwapa ujauzito  wanafunzi hasa wale wa sekondari wilayani Hai.

Sunday, 4 March 2018

MOTO WATEKETEZA VIBANDA VYA WAFANYA BIASHARA HAI

Na Latifa Botto
HAI
Zaidi ya vibanda saba vinavyotumika kama maduka katika eneo la Machine tools wilayani Hai mkoani Kilimanjaro vimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo huku wafanyabiashara wa eneo hilo wakidai kupata hasara kubwa.

Wazazi waaswa kutowatelekeza watoto wao Mashuleni

Na Davis Minja
HAI
Wazazi na Walezi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuacha tabia ya kuwatelekeza watoto katika shule wanazo soma pasipo kuwa nao karibu, hali inayosababisha  watoto kukosa upendo na malezi kutoka kwa wazazi.

MOTO WATEKETEZA VIBANDA VYA WAFANYA BIASHARA HAI

Na Latifa Botto
HAI

Zaidi ya vibanda saba vinavyotumika kama maduka katika eneo la Machine tools wilayani Hai mkoani Kilimanjaro vimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo huku wafanyabiashara wa eneo hilo wakidai kupata hasara kubwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Isa amesema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme uliosababisha vibanda saba kuteketea kwa moto.

Kwa upande wake mwenyekiti  wa kijiji cha wari ndoo ambaye pia ni shuhuda wa ajali hiyo ya moto bwana Emanuel muro wakati akizungumza na redio boma hai fm eneo la tukio wilayani hai amethibitisha pia kutokea kwa moto huo huku akidai hali halisi ya hasara iliyopatikana bado haijafahamika hadi sasa.

Ameongeza kwa kusema kuwa serikali iwafikirie wafanyabiashara waliopata hasara ya kuunguliwa na maduka yao pamoja na hilo serkali inapaswa kuwapa kibali cha kujenga majengo na si vibanda na kuboresha miundombinu haswa ya maji.

Kwa upande wa mmoja wa wamiliki wamaduka yaliyoungua Bw. Stanley Mushi amesema kuwa moto huo uliosababishwa na hitilafu ya umeme na kuliomba shirika la umeme  kuangalia suala hilo na kurekebisha miundombinu yake

Thursday, 1 March 2018

Polisi Yaimarisha ulinzi shuleni baada ya wanafunzi kufanya vurugu

Na Omary Mlekwa 

JESHI la polisi mkoa wa Kilimanjaro,limeimarisha  ulinzi na usalama katika shule ya sekondari ya Lyamungo iliyopo kata ya Machame Mashariki wilayani Hai kufuatia vurugu zilizojitokeza baina ya wanafunzi na walimu wa nidhamu wa shule hiyo.

Vurugu za wanafunzi zasababisha shule kufungwa kwa muda Hai

NA OMARY MLEKWA

HAI
 
SERIKALI wilaya Hai mkoani Kilimanjaro imeifunga shule ya Sekondari ya Lyamungo kwa zaidi ya wiki mbili baada ya Wanafunzi kufanya vurugu na uharibifu wakipinga mwenzao kufukuzwa shuleni hapo.

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...