Friday, 29 December 2017

WANACHAMA CCM KILIMANJARO WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WANAOJIUNGA NA CHAMA HICHO






Na Kija Elias, siha.

Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, kimewataka wanachama wa chama hicho kutowatenga wale wote wanaorejea ndani ya CCM, na badaala yake wawape ushirikiano.

Rai hiyo imetolewa jana na Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya wakati wa hafla ya kuwapokea madiwani watatu waliokuwa kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, pamoja na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Siha Dkt Godwin Molell  ambao wameamua kukihama chama hicho na kurejea ndani ya CCM. 

Mabihya aliwataka wanachama wa CCM kutokujiona wanyonge, pindi pale wanapowaona wanachama kutoka upinzani wakirejea ndani ya CCM, bali wawape ushirikiano kwani moja ya Ilani ya chama hicho ni kuwaunganisha watu pamoja.

Aidha Mabihya amewapongeza madiwani hao kwa uamuzi wao wa kurudi kwenye chama ambacho sera zake zinatekelezeka kuliko huko ambako walikuwa wakishindwa kuwaletea maendeleo wananchi wao kutokana na kutokuwa na serikali.

“Leo tumewapokea ndugu zetu hawa waliorudi ndani ya chama chetu, niwaombe wana CCm kuwapa ushirikiano wa kutosha ndugu zetu hawa na msijione wanyonge wapeni ushirikiano,”alisema.

Katika hatua nyingine chama hicho kimekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa na baadhi ya wanachama wa CHADEMA kuwa kimekuwa kikiwanunua wanachama ili warejee ndani ya CCM.

“Wako watu ambao wamekuwa wakiwaona watu wanaorejea CCM kuwa wamenunuliwa, hizo ni siasa za kupakana matope, dhamira zao ndizo zilizowatuma kurejea ndani ya CCM.

Alifafanua kuwa CCM haijawahi kupanga bei ya kumnunua mtu ili arejee ndani ya CCM, binadamu hana bei    

SERIKALI YAOMBWA KUIMARISHA ULINZI KWA WENYE ULEMAVU WA NGOZI






Na Kija Elias, Hai.


SERIKALI imeombwa kuongeza nguvu katika kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), ili nawao waendelee kuyafurahia maisha ya hapa ulimwenguni.


MADIWANI WILAYA YA HAI WAAPISHWA






Na, Riziki Lesuya
HAI

Madiwani wateule watatu  katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 26 mwaka huu wameapishwa leo ili kuungana na madiwani wengine katika kuwahudumia wananchi wa wilaya ya Hai.

Thursday, 28 December 2017

MAGUFULI AWAPA ONYO VIONGOZI WA SERIKALI



Rais John Magufuli amewasilisha fomu ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.

Wednesday, 27 December 2017

ASHIKILIWA KWA KUSAFIRISHA MIHADARATI







Na mwandishi wetu MOSHI

JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia mfanyakazi mmoja wa shirika la Umma la Mifuko wa Hifadhi ya Jamii (PPF, kwa tuhuma za kujihusiha na usafirishaji wa dawa za kulevya.

TRA KILIMANJARO YATEKELEZA AGIZO LA RAISI




Na mwandishi wetu. Hai. 

Mamlaka ya mapato TRA, mkoani Kilimanjaro, imetekeleza maagizo yaliyotolew hivi karibuni na  Rais Dkt John Magufuli ambayo iliwataka Mamlaka hiyo, kuhakikisha wanafunga mashine ambayo itadhibiti mapato yanayotokana na mizigo inayoingizwa ndani na nje ya nchi kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA. 

Wednesday, 13 December 2017

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO WAO





Na Anna Maduhu

Hai

Wazazi  na walezi wameshuriwa kuwa karibu na watoto wao katika kipindi hiki wanapokuwa likizo za shule kufungwa   ili kubaini changamoto mbalimbali zinzowakabili watoto pamoja na kuwaeleza madhara ya mimba za utotoni.

Tuesday, 12 December 2017

AOMBA MSAADA WA MALIPO YA MATIBABU BAADA YAKUCHOMWA KISU



Na mwandishi wetu

HAI

Mkazi wa kijiji cha Warisinde kata ya machame Kaskazini Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro Amemu Muru (47)ameomba msaada wa sh,800,000 anazodaiwa katika Hospitali ya Mkwarungo iliyopo machame wilayani humo ili aweze kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.


WENYEVITI WA VITONGOJI WATAKIWA KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA




Inspector Shabo wa kituo cha polisi Bomang'ombe wakati akizungumza katika kikao cha mamlaka ya mji mdogo wa Hai

Mwenyekiti wa mtaa wa Kingereka B, Saidi Seifu Mkambala wakati akizungumza katika kikao cha kamati ya mamlaka ya Mji mdogo wa Hai

WATAKIWA KUBUNI MIRADI YA MAENDELEO



HAI


WAUMINI wa dini ya Kiislamu Nchini wametakiwa kubuni miradi ya maendeleo itakayo wasaidia kukuza kipato cha familia na nchi kwa ujumla


Sunday, 10 December 2017

TANESCO YA FAFANUA KUHUSU KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA LUKU SIKU YA JUMAMOSI


Kaimu uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji (kushoto) na Kaimu meneja wa teknolojia na mawasiliano (TEHAMA) wa Tanesco,Demetruce Dashina (kulia) wakati wakizungumza na waandishi wa habari leo.

 

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka. 

MSANDO AWAFUNGUKIA UVCCM MBELE YA RAISI MAGUFULI

Wakili msomi, Alberto Msando ambaye alijiunga na (CCM) amefunguka na kuwachana vijana wa chama hicho UVCCM baada ya viongozi wake kumdanganya  Dkt. John Pombe Magufuli juu ya idadi wa vijana wao.

Saturday, 9 December 2017

NAIBU WAZIRI AWAPONGEZA WANANCHI KWA KUCHANGIA MAENDELEO


Moja ya Mabweni katika Shule ya Sekondari Harambee Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro 


Na Riziki Lesuya
HAI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda amefurahishwa na kuridhishwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo Wilayani Hai na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji  Yohana Sintoo  kwa usimamizi mzuri unaoendana  na thamani ya fedha iliyotumika.

SERIKALI KUIFANYIA MAREKEBISHO SHERIA YA MAKOSA YA KUJAMIIANA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Harambee katika ziara yake Wilaya ya Hai 

Na. Adrian Lyapembile
HAI

Serikali imejipanga kukabiliana na matukio ya mimba za utotoni kwa kufanya marekebisho ya sheria ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998.
Dhamira hiyo ya Serikali imebainishwa na Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda katika mkutano aliofanya na watumishi wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Monday, 20 November 2017



HAI YAJIPANGA KUSAIDIA VIKUNDI VYA UFUGAJI NYUKI

NA OMARY MLEKWA NA QUEEN NDOSY

HALMASHAURI ya wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro imejipanga kuviwezesha vikundi vya ujasilimali vinavyojishughulisha na uzalishaji wa asali ili viweze kuzalisha kwa ubora hali ambayo itasaidia kujiongezea kipato. 




NGOMBE ELFU 68 KUPIGWA CHAPA WILAYANI  HAI.


Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ya Hai Ndg, Yohana Sinto Akizungumza na Baadhi ya wafugaji katika kijiji cha Sanya Station Kata ya Kia Wakati alipotembelea kijiji hicho kujionea zoezi la upigaji chapa kwa ng"ombe wawafugaji hao. (picha na Omary Mlekwa)
 
Zoezi la upigaji chapa ng'ombe Wilayani Hai likiwa linaendelea katika kijiji cha Sanya Station Mkoani Kilimanjaro (pcha na Omary Mlekwa)

 NA OMARY MLEKWA NA QUEEN NDOSY, -Hai

ZAIDI ngombe elfu 68 zinatarajiwa kupigwa chapa katika zoezi lililoanza kwenye Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro  ili kutekeleza Agizo la wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo linatarajiwa kukamilika Desemba 30 mwaka huu.


Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...