Na Kija Elias, siha.
Chama Cha Mapinduzi mkoa wa
Kilimanjaro, kimewataka wanachama wa chama hicho kutowatenga wale wote
wanaorejea ndani ya CCM, na badaala yake wawape ushirikiano.
Rai hiyo imetolewa jana na
Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya wakati wa hafla ya
kuwapokea madiwani watatu waliokuwa kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema, pamoja na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Siha Dkt Godwin Molell ambao wameamua kukihama chama hicho na
kurejea ndani ya CCM.
Mabihya aliwataka wanachama
wa CCM kutokujiona wanyonge, pindi pale wanapowaona wanachama kutoka upinzani
wakirejea ndani ya CCM, bali wawape ushirikiano kwani moja ya Ilani ya chama
hicho ni kuwaunganisha watu pamoja.
Aidha Mabihya amewapongeza
madiwani hao kwa uamuzi wao wa kurudi kwenye chama ambacho sera zake
zinatekelezeka kuliko huko ambako walikuwa wakishindwa kuwaletea maendeleo
wananchi wao kutokana na kutokuwa na serikali.
“Leo tumewapokea ndugu zetu
hawa waliorudi ndani ya chama chetu, niwaombe wana CCm kuwapa ushirikiano wa
kutosha ndugu zetu hawa na msijione wanyonge wapeni ushirikiano,”alisema.
Katika hatua nyingine chama
hicho kimekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa na baadhi ya wanachama wa CHADEMA
kuwa kimekuwa kikiwanunua wanachama ili warejee ndani ya CCM.
“Wako watu ambao wamekuwa
wakiwaona watu wanaorejea CCM kuwa wamenunuliwa, hizo ni siasa za kupakana
matope, dhamira zao ndizo zilizowatuma kurejea ndani ya CCM.
Alifafanua kuwa CCM haijawahi
kupanga bei ya kumnunua mtu ili arejee ndani ya CCM, binadamu hana bei
No comments:
Post a Comment