![]() |
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Harambee katika ziara yake Wilaya ya Hai |
Na. Adrian Lyapembile
HAI
Serikali imejipanga kukabiliana na matukio ya mimba za utotoni kwa kufanya marekebisho ya sheria ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998.
Dhamira hiyo ya Serikali imebainishwa na Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda katika mkutano aliofanya na watumishi wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Aidha ameitaka jamii kwa ujumla kushirikiana kupiga vita matukio ya mimba za utotoni na kwa wanafunzi ambayo yameonekana kuongezeka kwenye mkoa wa Kilimanjaro na kubainisha kuwa wazazi wana mchango mkubwa katika kutokomeza matukio hayo kwani ni kesi chache zinazofikishwa mahakamani na nyingi hazitolewi hukumu kwa kukosekana ushahidi.
Amewataka watumishi kuwa mabalozi wa kuwaelimisha wazazi kuhusu malezi ya watoto na zaidi kujiepusha na namna yoyote ya ushiriki kwenye kuharibu ushahidi pale inapotokea mtoto amepewa mimba bali washiriki kuhakikisha haki inatendeka na wahalifu wanapata adhabu wanayostahili.
No comments:
Post a Comment