Na mwandishi wetu. Hai.
Mamlaka ya mapato TRA, mkoani
Kilimanjaro, imetekeleza maagizo yaliyotolew hivi karibuni na Rais
Dkt John Magufuli ambayo iliwataka Mamlaka hiyo, kuhakikisha wanafunga mashine
ambayo itadhibiti mapato yanayotokana na mizigo inayoingizwa ndani na nje ya
nchi kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Akiongea wakati wa ufungaji wa
mashine hiyo mpya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, alisema kuwa uwepo
wa mashine hiyo pia utasaidia uwezekano wa kupotea kwa mapato ya serikali
katika uwanja huo.
“Mashine hii itasaidia
kudhibiti aina zote za upotevu wa mapato ya serikali, kwani inaweza kukagua
mizigo inayoingizwa nchini na ile inayotoka n kufanyiwa makadirio mbalimbali
kwa ufanisi zaidi”, alisema.
Aidha alisema mashine hiyo italeta
uwazi na utoaji wa huduma ulio bora na wenye kuzingatia haki.
Aidha aliipongeza TRA kwa jitihada
zake za makusudi zinazolenga kuziunga juhudi za Rais Dkt Magufuli katika
kulinda mapato ya Taifa.
Kwa upande wake Meneja wa TRA Mkoa
wa Kilimanjaro, Msafiri Mbibo, alisema kuwa mashine hiyo mpya itasaidia
kuboresha usalama wa raia kwa kuhakikisha mizigo yote inakaguliwa ili kujua
inayo stahiki zote.
“Pia zitasaidia kurahisisha shughuli
za wasafiri wanaoingia na kutoka nje ya nchi kwa kutumia uwanja wa ndege na
mipaka yetu”, alisema.
Alisema pia zitasaidia kutoa huduma
za haraka kwa wasafiri na mali zao, waagizaji wa bidhaa, mizigo na mali
mbalimbali na wale wanaopeleka nje ya nchi.
“Mashine hii itasaidia
kugundua endapo abiria atakuwa amebeba dawa za kulevya, madini kinyume cha
sheria, nyara za serikali kama vile pembe za ndovu, vilivyofichwa ndani ya
begi”, alisema.
Kwa upande wake Kimu Mkurugenzi wa
uendeshaji wa kiwanja cha ndege KIA Mhandisi, Martin Kinyamagoha, alisema kuwa
mshine hiyo itasaidia sana kupunguza msongamano wa abiria katika uwanja huo
kutokana iliyokuweko moja na ilikuwa ni ndogo.
Nae Mkuu wa TRA uwanja wa KIA Elias
Njata, alisema kuwa mashine hiyo itasaidia usafirishaji na utorosha madini na
nyara zingine za serikali ikiwemo pembe za ndovu.
No comments:
Post a Comment