Na mwandishi wetu
HAI
Mkazi wa kijiji cha Warisinde kata ya machame Kaskazini
Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro Amemu Muru (47)ameomba msaada wa sh,800,000
anazodaiwa katika Hospitali ya Mkwarungo iliyopo machame wilayani humo ili
aweze kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.
Akizungumza na Mwandishi aliko lazwa katika hospitali hiyo,alisema
anadaiwa fedha hizo kwa ajili ya matibabu aliyoyapata ili aweze kuruhusiwa
kutoka hospitalini hapo.
Muru alisema kuwa amerusiwa kutoka hospitali wiki mbili zilizopita lakini fedha
za kulipa amekosa hivyo kuomba wananchi
mwenye nia ya kumsaidia kuilipa ili aweze kutoka
Mwanamke huyo alifikishwa Hostalini hapo Novemba 10 mwaka
huu baada ya kuchomwa kisu cha mkono wakati akimuokoa binti yake wa kidato cha
pili asibakwe na muhuza chipisi
Afisa Tarafa Machame Nsajigwa Nadagile,alisema kwamba mama
huyo amekuwa akimpigia simu mara kwa mara kwa ajili ya kuomba msaada wa kulipa
fedha za matibu
Kiongozi mmoja wa
Hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe,alisema wanamdai mama huyo na anachotakiwa
ni kulipa iliaweze kuruhusiwa kurudi nyumbani ,lakini jinsi anavozidi kukaa
hapo fedha nazo zinaongezeka
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji hicho Nasoro Mushi alikiri
kuwa mama huyo alichomwa kisu kwenye kiwako cha mkono na kijana anayefahamika
Nasoro Ramadhani (24)msambaa mkazi wa kijiji hicho ambaye pia ni muhuza chipsi
,na kwa sasa jambo hilo lipo kwenye vyombo vya seria
No comments:
Post a Comment