Na mwandishi wetu MOSHI
JESHI
la polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia mfanyakazi mmoja wa shirika la Umma
la Mifuko wa Hifadhi ya Jamii (PPF, kwa tuhuma za kujihusiha na usafirishaji wa
dawa za kulevya.
Akidhibitisha
kukamatwa kwake, kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Hamis Issa, alimtaja mtu
huyo kuwa ni Anitha Oswald (32) ambaye ni mfanyakazi wa Shirika mifuko wa
hifadhi wa PPF, mkoani Kilimanjaro.
“Askari
wakiwa doria walimkamata Anitha Oswald, ambaye ni mkazi wa Karanga, Manispaa ya
Moshi, akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 216 na gramu
370”, alisema kamanda Issa.
Alisema
kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa akisafirisha mirungi hiyo kwa kutumia gari lake
analolimiliki mwenyewe lenye namba za usajili T 674 DLB, aina ya Toyota Sienta
rangi ya silva.
Kamanda
Issa alisema Anitha Oswald alikamatwa eneo la Majengo kwa Mtei Disemba 19,
mwaka huu, akiwa anatokea Njia Panda ya Himo kuchukua mzigo huo.
Aidha
kamanda Issa alisema kwamba usafirishaji wa dawa za kulevya bado ni changamoto
kubwa ambapo alielezea kusikitishwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa Umma
kujihusisha na usafirishaji huo.
“Jeshi
la polisi mkoani hapa liko makini, operesheni inaendelea na hatutamvumilia mtu
yeyote ambaye atabainika kujihusisha na biashara hii”, alisema.
Hata
hivyo kamanda aliongeza kusema kwamba jeshi hilo la polisi mkoni humo, bado
linaendelea kumtafuta dereva wa gari hilo, ambaye alikimbia baada ya
kulitelekeza gari alilokuwa akiliendesha baada ya kugonga mti katika jitihada
za kuwakimbia polisi.
No comments:
Post a Comment