Monday, 20 November 2017



NGOMBE ELFU 68 KUPIGWA CHAPA WILAYANI  HAI.


Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ya Hai Ndg, Yohana Sinto Akizungumza na Baadhi ya wafugaji katika kijiji cha Sanya Station Kata ya Kia Wakati alipotembelea kijiji hicho kujionea zoezi la upigaji chapa kwa ng"ombe wawafugaji hao. (picha na Omary Mlekwa)
 
Zoezi la upigaji chapa ng'ombe Wilayani Hai likiwa linaendelea katika kijiji cha Sanya Station Mkoani Kilimanjaro (pcha na Omary Mlekwa)

 NA OMARY MLEKWA NA QUEEN NDOSY, -Hai

ZAIDI ngombe elfu 68 zinatarajiwa kupigwa chapa katika zoezi lililoanza kwenye Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro  ili kutekeleza Agizo la wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo linatarajiwa kukamilika Desemba 30 mwaka huu.


Hayo yamebaishwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ndg Yohana Sinto wakati  akizungumza na wafugaji wa kijiji cha Sanya Station Kata ya Kia alipotembelea kujionea zoezi hil.

Alisema kuwa kuna kila sababu kwa wakazi wa wilaya ya Hai haswa wafugaji kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo ili kuwezesha wanyama wao kupigwa chapa kutokana na umuhimu wa zoezi hil.

< Zoezi hili ni muhimu ni  sana kwa wakazi wa wilaya yetu ya Hai kwani tunatambua jinsi mifugo kutoka nje imekuwa ikitusumbua kutokana na kutokuwa na alama inayoweza kutambulisha mifugo yetu , naomba tutumie fursa hii vizuri ;alisema Sintoo.

Alisema kuwa kukamilika kwa zoezi hilo itasaidia kutambua mifugo iliyopo kwani wilaya imekuwa na migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji kutokana na wimbi kubwa la mifugo kutoka wilaya za jirani na hata wafugaji kutoka  nje kuvamia mashamba ya wakulima kwa ajili ya malisho.

Hata hivyo aliwataka wafugaji wote kutoa mifugo yao na kupigwa kwa muda huu na mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo wataanza kuwachukulia hatua wale ambao watashindwa kutekeleza agizo hil.

Kwa upande wake afisa mifugo wa wilaya ya Hai, Elia Machange tangu kuanza kwa zoezi hilo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kuni za kuchomea chombo kimachumika kwa ajili ya kupigia chapa ngombe.

Aidhani amesema kutokana na matumizi makubwa ya kuni wamejipanga kuhakikisha kuwa zoezi hilo halikwami kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji kutoa ushirikiano wao wa ili kukabiliana  tatizo hilo na huduma iendeele kutolewa kwa muda wote.

Nae  kiongozi wa kimila wa kabila wa wafugaji katika eneo hilo Thomas Sinyoki  alisema zoezi litasaidia kujua ngombe watakaovamia maeneo yao kwani mifugo yao itakuwa na chapa ya wilaya ya Hai

Sinyoki alisema pia kupigwa chapa kwa ngombe hao itasaidia kuondoa mwingiliano wa mifugo kwa wilaya nyingine jambo ambalo litawasaidia katika kuhifadhi sehemu za malisho.

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...