HAI
WAUMINI wa dini ya Kiislamu Nchini wametakiwa kubuni miradi
ya maendeleo itakayo wasaidia kukuza kipato cha familia na nchi kwa ujumla
Wito huo umetole na
Shekh Hamis Ame kutoka Dare saalama wakati wa Kongamana la siku tano kiislamu
lililofanyia Bomang'ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro,lengo kubuni miradiya maendeleo na kuachana na
makudi yasiyo eleweka katika dini
Ame alisema ni vyema Waislamu watambue umuhimu wa kushiriki
kuanzisha miradi mbali mbali ya maendeleo kama kujenga Hospitali , shule na viwanda zitakazo
wasaidia kukuza kipato na kuleta
maendeleo
''Alisema Waislamu wa frusa nyingi za kuleta maendeleo wamebaki
nyuma kutokana na kushindwa kujitoa kuchangia fedha za kutosha kwa ajili ya
kuanziasha miradi ya maendeoleo''alisema Ame
Aidha aliwataka waumini hao kusoma na kuielewa dini hiyo
iliwasije tumbukia katika makundi mabaya ambayo yanajinasibisha na dini hiyo na
kusababisha sintofahamu
''Kuna makundi hapa duniani yanafanya mambo ambayo ni
kinyume na mafundisho ya dini yanatakiwa kuondoshwa mara moja au kuyapunguza
kabla hayajaleta mazara''alisema Ame
Kwa upande wake Abdlah Juma immamu wa msikiti wa Abuu uliopo
Bomang'ombe aliwataka waislamu kuzingatia elimu ili kwenda sambamba na Tanzania
ya viwanda.
Waumini tunatakiwa kusoma na kuwa wabunifu wa mawazo mapya
yatakayo waletea maendeleo bora na kukuza uchumi wetu na Nchi kwa ujumla kuliko
kukaa na kupika majungu yasiyo na tija.
No comments:
Post a Comment