Na Anna Maduhu
Hai
Wazazi na walezi wameshuriwa
kuwa karibu na watoto wao katika kipindi hiki wanapokuwa likizo za shule
kufungwa ili kubaini changamoto
mbalimbali zinzowakabili watoto pamoja na kuwaeleza madhara ya mimba za
utotoni.
Akizungumza katika kipindi cha siku mpya kinachorushwa na
Radio Boma Hai fm leo mwenyekiti wa dawati la jinsia na watoto
wilayani Hai, Happyness Eliufoo alisema
endapo wazazi watakuwa karibu na watoto wao katika kipindi hiki cha likizo itasaidia
kupunguza tatizo la mimba pia watajua matatizo yanayowakabili watoto wao.
Eliufoo amesema kuwa tatizo la baadhi ya wazazi au walezi
kushindwa kuwa karibu na watoto limechangia zaidi watoto kufanyiwa vitendo vya
ukatali ikiwemo kupewa mimba kutokana na baadhi kushindwa kuwapatia elimu ya
madhara ya mimba za utotoni.
Nae afisa kutoka shirika lisililo la kiserikali la Ajiso la
Mjini Moshi ,Tatu Mruthu amesema kuwa ni vema wazazi au walezi
wakatenga mda wa kukaa na watoto wao hali ambayo itasaidia kutambua na kujua
changamoto wanazokabiliana nazo wawapo nyumbani tofauti na kipindi walipokuwa
shuleni.
Kwa upande wake , afisa ustawi wa jamii kutoka wilaya ya
Hai, Michael Mahundi licha ya wazazi kukosa mda wa kukaa na watoto wao bado jamii imekosa ushirikiano
na kutoa taarifa za matukio mbali mbali ya ukatili wanaofanyiwa watoto nyumbani
jambo ambalo limechangia kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukatli kwenye jamii.
Akichangia kwa njia ya simu katika kipindi hicho, mkazi wa mtaa
wa Uzunguni Praygodi Muro alisema tatizo la mimba shuleni limechangiwa sana na umbali kutokana
na baadhi ya watoto kutembea zaidi ya kilometea tatu kufuata shule ambapo
wanafunzi huweza kukutana na vishawishi wakiwa njiani.
No comments:
Post a Comment