Na,
Riziki Lesuya
HAI
Madiwani wateule watatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai
waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 26 mwaka huu wameapishwa
leo ili kuungana na madiwani wengine katika kuwahudumia wananchi wa wilaya ya
Hai.
Madiwani walioapishwa ni Mhe.
Martin Munisi wa kata ya Machame Magharibi, Mhe. Salehe Msengesi wa kata ya Weruweru
na Mhe. Nasibu Mndeme kutoka kata ya Mnadani.
Madiwani hao walikula kiapo
hicho mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Hai Regina Moshi Katika
ukumbi wa Halmashauri likishuhudiwa na wajumbe wa Baraza la madiwani, wataalamu
wa halmashauri pamoja na wananchi waliohudhuria kwenye kikao hicho.
Awali akifungua kikao cha Baraza
la Madiwani wa Halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Helga Mchomvu
amewakaribisha madiwani walioapishwa na kuwataka kuongeza nguvu katika jukumu
la kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Hai kwa kuzingatia kanuni na taratibu za
halmashauri.
Aidha mchomvu amewataka
madiwani hao kutambua kuwa halmashauri inaongozwa kwa kanuni na si vinginevyo
na kwamba kila mmoja anao wajibu wa kuchangia na kuwa mbunifu katika kuiletea
maendeleo Halmashauri.
Amesema kuwa swala la siasa
lilimalizika kwenye kipindi cha kampeni na sasa ni wakati wa kutekeleza
kilichoahidiwa kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment