Monday, 20 November 2017



HAI YAJIPANGA KUSAIDIA VIKUNDI VYA UFUGAJI NYUKI

NA OMARY MLEKWA NA QUEEN NDOSY

HALMASHAURI ya wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro imejipanga kuviwezesha vikundi vya ujasilimali vinavyojishughulisha na uzalishaji wa asali ili viweze kuzalisha kwa ubora hali ambayo itasaidia kujiongezea kipato. 




Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Ndg Yohana Sintoo aliyasema hayo wakati alipotembea kiwanda cha mradi wa asali cha Hai (HABECO)kilichopo wilayani hapa cha  kusafisha na kuhifadhi asali cha  ufugaji wa nyuki na kupanua uzalishaji wa asali.

Kwa upande mratibu wa mradi huo,  Japheti Mmari alisema mradi huo umewasaidia wanavikundi wengi kutoka wilaya za Hai, Rombo na Siha kutokana na kununua asali kwao kwa ajili ya kuja kuzisafisha kwa mashine ya kisasa .


Mmary alisema kuwa mpaka sasa wameshindwa kukusanya asali yote kutoka kwa wazalishaji  kutokana na kutokuwa na mtaji wa kutosha na kuomba serikali kuwasaidia kuwaongezea  mtaji ili waweze kukusanya asali kwa wingi

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...