Saturday, 28 April 2018

Hai yapanda miti kusheherekea miaka 54 ya Muungano



Katibu Tawala Wilaya ya Hai Bi. Upendo Wella akiongoza zoezi la upandaji miti katika kijiji cha Mtakuja kata ya Kia.

Kameshina wa scout Mkoa wa Kilimanjaro Broity Maktora akishiriki zoezi la upandaji miti.

Afisa maliasili Wilaya ya Hai Bw. Mbayan Mollel akishiriki zoezi la upandaji miti kusheherekea miaka 54 ya muungano.

''Wazazi Wapelekeni Watoto Kupata Chanjo''DC HAI

Mkuu wawilaya ya Hai Mh. Onesmo Buswelu wakati akizindua chanjo ya polio kwa watoto katika Hospital ya Wilaya ya Hai

Thursday, 26 April 2018

HAI ya sheherekea Muungano kwakupanda miti

Na Zaina Andrew na Praygod Munis

HAI

Wakati maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyo fanyika leo mjini Dodoma, halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamesherehekea sikukuu hiyo  kwa kupanda miti katika kata ya Kia kijiji cha Mtakuja.

Katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wella amesema kutokana na watu kushidwa kwenda kwenye maadhimisho hayo mjini Dodoma hivyo ameona ni vyema kutumia muda huo  kwa ajili yakupanda miti ili kuboresha mazingira ya wilaya ya Hai pia taifa kwa ujumla, sambamba na kauli mbiu ya "TANZANIA YAKIJANI INAWEZEKANA  PANDA MITI KWA MAENDELEIOYA VIWANDA" .

Naye kamishina  wa scout mkoani Kilimanjaro Broity Maktora amesema kuwa wameadhimisha muungano kwa kupanda miti kwa lengo la kuboresha amani ya Taifa la Tanzania pia   kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa  kuifanya Kilimanjaro kuwa ya kijani.

Hata hivyo afisa maliasili wa wilaya ya Hai Mbayani Moleli ameeleza kuwa kutakana na changamoto nyingi zinazowakabili zaidi kwenye utunzaji wa miti hiyo kwa baadhi ya wafugaji ila ameeleza kuwa wametoa elimu kwa wanajamii na pia wataendelea kutoa elimu hiyo ili kuweza kuimarisha na kuboresha utunzaji wa miti hiyo .

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja  Teheraki Kipara Moleli amezungumza kuwa kutokana na elimu iliyotolewa kwa wamajamii  wamekuwa na uelewa wa umuhimu wa kupanda miti kwani wanajamii hao  wanajitihada kubwa ya kuzidi kupanda miti kwenye makazi yao hivyo  wanatarajia mabadiliko makubwa ya uboreshwaji wa  mazingira.

Saturday, 21 April 2018

DC ahimiza shughuli za kimaendeleo





Mkuu wa Wilaya Ya Hai Mh. Onesmo Buswelu katikati akisikilza maelezo kutoka kwa kamati ya shule ya sekondary Longoi iliyopo kata ya  weru weru wilayani Hai mara baada yakufika shuleni hapo.


Kamati ya shule ya Sekondary Longoi wakimsikiliza kwa umakini mkuu wawilaya ya Hai Onesmo Buswelu baada yakutembelea shuleni hapo.

DC HAI AAGIZA MTO KUFANYIWA USAFI BAADA YA MAFURIKO KUTOKEA



Meneja wa TARURA Wilaya ya Hai Mhandisi Charles Marwa (kulia) akitoa maelezo katika kijiji cha sanya station katika kata ya Kia baada yakukumbwa na mafuriko.

Mkuu wa wilaya ya Hai Mh. Onesmo Buswelu Akitoa maelekezo kwa viongozi wa kijiji cha sanya station, pamoja na maafisa mazingira wilaya mara baada ya kijiji hicho kukumbwa na mafuriko.

Mkazi wa kijiji cha sanya station akizungumzia athari ziliz
otokea mara baada ya mafuriko kutokea kijijini hapo.




Eneo ambalo mto umeacha njia yake rasmi nakutengeneza mto mwingine pembeni mara baada ya mvua kubwa kunyesha katika kijiji cha sanya station kata ya Kia wilayani Hai( Picha zote na Davis Minjer)


Wednesday, 11 April 2018

TASAF yazidi kuwanufaisha kaya masikini Hai


Na Omary Mlekwa

HAI

WANUFAIKA wa mpango wa kunusuru kaya maskini unaondeshwa na mfuko wa jamii (TASAF) wameshauriwa  kutumia fedha wanazopata kuanzisha shughuli za ujasiriamali ili kuondokana na hali tegemezi .

Wananchi Watakiwa Kutunza Miti Wanayootesha

Na Omary Mlekwa Hai


MKUU wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Onesmo Buswelu amewataka wananchi kutunza miti inayooteshwa katika kipindi hiki cha mvua ili iweze kukua na kukabiliana na hali ya ukame kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...