Tuesday, 13 February 2018

UKOSEFU WA FEDHA WACHANGIA HALMASHAURI YA SIHA KUSHINDWA KUFIKIA MALENGO YA UOTESHAJI MITI

Na Omary Mlekwa
Siha

UKOSEFU wa fedha za kuboresha kitalu cha miti katika Halmashauri ya Siha imechangia kushindwa kufikia malengo ya uoteshaji miti kwenye maeneo mbali mbali katika wilaya hiyo.



Ukosefu huo unatokana na kushindwa kutolewa kwa fedha zinazokadiriwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha husika.

Hayo yalibainishwa katika kikao cha baraza la  Halmashauri hiyo ambapo katika mwaka wa fedha wa 2017 /2018 kiasi cha shilingi milioni 18 zilitarajiwa kutumika kwa ajili ya kuboresha kitalu cha miche miti kikichopo shamba la miti la westi Kilimanjaro tawi la Sanya Juu.

Diwani wa kata ya Karansi ,Dancan Urassa alisema Halmashauri kushindwa kuhudumia kitalu hicho itapelekea kushindwa kukabiliana na hali ya ukame pamoja na kuboresha Mazingira
"Kitalu chetu kilikuwa  kikihudumia wananchi wengi sana hata tasisi za dini ,shule na hata watu binafsi ni bora fedha zinazowekwa kwenye bajeti ziwe zinatengwa "alisema Urassa

Nae Diwani wa kata ya livishi Witson Nkini alisema suala la  uoteshaji miche kwenye kitalu ni muhimu sana na kuwataka watendaji kuacha mzaha katika suala hilo.

Kufuatia hali ,Mwenyekiti wa Halmashauri ,Frank Tarimo alimtaka mkurugenzi kutafuta pesa ambazo zitaweza kutumika  kwa ajili ya uboreshaji wa kitalu

Kwa upande wake Afisa Misitu,Lazaro Mwaluko alisema hadi mwishoni  mwa robo  ya pili wamepokea kiasi cha shilingi laki  mbili tu
" Pamoja na kitalu kukosa fedha za kukiendesha bado tumeweza kuotesha  miti kwa kushirikiana na wadau wengine wa Mazingira "

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...