Tuesday, 13 February 2018

USHIRIKIANO IDARA YA ELIMU SEKONDARI NA WADAU WA ELIMU WACHANGIA ONGEZEKO LA UFAULU

Na Omary Mlekwa
Siha

USHIRIKIANO kati ya idara ya Elimu sekondari na wadau wa elimu  umechangia kuongeza  hali ya ufauli kwa watahiniwa wa mtihani kidato cha nne  katika Halmashauri ya Siha Mkoani Kilimanjaro.
 
Halmashauri hiyo imeweza kushika nafasi ya pili kimkoa na nafasi ya 16 kitaifa mwaka 2017 ikilinganishwa na nafasi ya 5 kimkoa na ya 40 kitaifa mwaka 2016.

Akitoa taarifa  katika baraza la  madiwani ,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Frank Tarimo alisema jitihada zilizoonyesha na idara ya Elimu Sekondari zinahitajika ili kuendelea kufanya vizuri,

"Idara ya elimu  pamoja na walimu wamefanya kazi nzuri sana ambapo wameweza kuboresha sana matokeo ya mwaka huu ambapo halmashauti yetu tumeshika nafasi ya pili kimkoa na ya kumi na sita  kitaifa kati ya Halmashauri ya 194" alisema Tarimo

Alisema katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne  mwaka 2017 jumla ya watahiniwa 912 walifauli katika  daraja la kwanza hadi la nne kati ya watahiniwa 1137 waliofanya mtihani .

"Wilaya yetu imeweza kuongeza ufaulu kwa kiwango kikubwa kwani katika mwaka 2016 tulifanya vibaya ambapo shule moja iliingia nafasi ya kumi bora kwa kushindwa kufanya vizuri" alisema

Kwa upande wake ,kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Saro aliwataka kuhakikisha kuwa wanawafuatikia wanafunzi  ambao wamekuwa watoro pamoja na kuwashauri wazazi kuwapatia huduma zote zinazostah

Alisema wilaya hiyo,inajumla ya shule kumi na saba ambapo shule 13 zinamilikiwa na serikali huku shule 4 zikimilikiwa  na taasisi binafsi .

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...