Na Omary Mlekwa
Siha
Siha
WAZIRI wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema fedha zinazotolewa na serikali katika Halmashauri ya Siha sio rushwa kutokana na jimbo hilo kuwa kwenye mchakato wa uchaguzi bali ni utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015.
![]() |
WAZIRI wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu,akimnadi mgombea Ubunge Jimbo la Siha Dr Godwin Molel kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM.(picha na Omary Mlekwa) |
Akihutubia wananchi wa kijiji cha Louwang kata ya Donyomurwa katika mkutano wa kumnadi Mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi CCM, Dkt Godwin Moleli alisema serikali inadhamiria kuboresha huduma mbalimbali za kijamii
Alisema serikali itaendelea kuleta fedha za utekelezaji wa miradi na kinachohitaji ni wananchi kuendelea kuiamini serikali ya awamu ya tano kwa kumchagua Mgombea wa CCM, Dkt Moleli.
Alisema kuwa ,kabla ya kujiuzulu nafasi ya Ubunge Dkt Moleli licha ya kuwa alikuwa mbunge wa upinzani alimwomba fedha za ujenzi wa kituo cha Afya ambapo serikali iliahidi kumpatia kiasi cha shilingi milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Naibilie kata ya Makiwaru
Alisema ,serikali ilikuwa ikiipatia hospitali ya wilaya ya Siha kiasi cha shilingi i Milioni 17 kwa mwaka kwa ajili ya madawa lakini kwa sasa inapokea kiasi cha shilingi milioni44 kwa mwaka
Alisema kuwa serikali imeongeza fedha katika Vituo vya afya 2 na zahanati 9 ambapo ilikuwa ikipokea shilingi Milioni 38 mwaka ila kwa sasa fedha hizo zimeongezeka na kufikia kiasi cha shilingi milioni 175 mwaka
No comments:
Post a Comment