Saturday, 10 February 2018

WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUANZISHA JUKWAA LA WAZAZI NA WAALIMU

Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Hai, Julius Kakyama akisisitiza jambo kwenye kikao cha walimu na wazazi wa wanafunzi. (Picha zote na Praygod Munisi)


 Na Praygod Munisi 
HAI

Wakuu washule za secondary za serikali wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuanzisha jukwaa la wazazi na waalimu ndani ya mwezi mmoja ikiwa ni sehemu ya majukumu yao ili kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya shule na wanafunzi.

Hayo yamesemwa na afisa elimu secondary wilaya ya Hai Bw.Julius Kakyama wakati akizungumza na wazazi katika kikao kilichofanyika katika shule ya secondary Hai Day iliyopo mjini Bomang’ombe, ambapo amesema kwamba kulingana na majukumu ya mkuu wa shule jukwaa hilo la wazazi na waalimu litasaidia kujadiliana maswala mbalimbali kuhusu maendeleo ya shule na wanafunzi katika kutekeleza nyaraka mbalimbali ya elimu msingi bila malipo.

Aidha Kakyama amewakumbusha waalimu jukumu la kuwa na nidhamu na maadili ili wanayoyasema kwa wanafunzi waige huku akiwakumbusha wazazi kufuatilia maendeleo ya masomo ya watoto wao shuleni na kuakikisha wanaudhuria mashuleni huku wakiwalea watoto hao katika maadili mema wakishirikiana na waalimu jambo ambalo litsaidia kupunguza utoro mashuleni nakuongezeka kwa kiwango cha ufaulu.

"yote kwa yote waalimu wakae darasani watoe kazi,yaani mimi nawataka watoto wakose muda,wapate muda wakusoma tu hizi ziro tunaziondoa mabegi yachekiwe kila mwalimu akiingia darasani ajue mtoto gani yupo,kila mwalimu anapaswa kuwa na daftari la atendensi ya darasa lake kwa watoto wake kila akiingia ajue watoto wote wapoo’’ amesema Kakyama.

Kwa upande wao wazazi wamelalamikia kukithiri kwa utoro na uzururaji wawanafunzi nje ya eneo la shule muda wa masomo na kuwepo kwa wanafunzi wanaomiliki simu shuleni hapo kinyume na taratibu, huku wakioji utaratibu uliopo unaowaruhusu wanafunzi kuwa nje ya eneo la shule muda wa masomo jambo lililopelekea kuomba kuwekewa uzio katika shule hiyo, na kuwaomba waalimu kushirikiana nao ilikuakikisha wanafunzi wanakuwepo shuleni hapo muda wote wa masomo,jambo lilopelekea afisa elimu kumwagiza mkuu wa shule hiyo kuchukua hatua mara moja kwa wanafunzi watoro na mwanfunzi atakae kamatwa na simu shuleni hapo .  
"watoto wale wa bweni huwa tunawapa simu ili kumonita kwasababu pengine wanaenda mbali na wakifika huwa wana kabidhi,lakini Yule mtoto  anaekuja anarudi jioni unampa simu ya nini,yakufanya nini?hizo simu zote zinapokamatwa ni kupasua ndio msimamo wa serikali hatuna msimamo mwingine zaidi ya huo’’amesema Kakyama.

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...