Mwenyekiti wa
Mtandao wa Redio za Jamii Tanzania –TADIO ndugu PROSPER KWIGIZE akizungumza na washiriki wa mafunzo katika ukumbi wa TBA
Mkufunzi Mwandamizi wa Radio za
kijamii kutoka Shirika la
Umoja Wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni –UNESCO Bi Rose Mwalimu akifundisha.
Waandishi wa Habari kutoka Redio za
Kijamii Tanzania wametakiwa kutumia
fursa zinazotolewa na Shirika la
Umoja Wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni –UNESCO- ili kuleta
mabadiliko kwa Jamii.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa
Mtandao wa Redio za Jamii Tanzania –TADIO ndugu PROSPER KWIGIZE katika
mafunzo yanayoendelea mjini Dodoma na kwamba mafunzo ya kitaaluma kama hayo utolewa kwa kulipia
ila UNESCO utoa mafunzo kama hayo bila malipo yoyote.
Amesema ni vyema kuthamini na
kuzingatia elimu wanayoipata waandishi
katika mtandao wa TADIO na kuifanyia
kazi kwa manufaa ya jamii.
Naye Mkufunzi Mwandamizi wa Radio za
kijamii kutoka Shirika la
Umoja Wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni –UNESCO Bi Rose Mwalimu amewataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini kutoingilia uhuru wa wanahabari katika vituo vyao kwa sababu
vinaongozwa na sera na misingi ya taaluma ya habari.
Amesema ni vyema wanahabari wakawa
huru katika kutimiza wajibu wao
kitaaluma ili kuihudumia jamii na
kujiepusha na masuala binafsi.
No comments:
Post a Comment