Na Elisha Eliakimu HAI
Katibu tawala wilaya ya Hai Bi Upendo Wela amewataka mahakimu kutumia vizuri
tekinolojia ya tehama hususani mitandao ya kijamii katika kufanya shughuli zenye maendeleo.
Ameyasema hayo katika kilele cha maadhimisho
ya siku ya sheria nchini kwa mwaka huu yenye kauli mbiu isemayo"matumizi ya tehama katika utoaji
wa haki kwa wakati na kwa kuzingatia
maadili''
Pia Wela amesema ni wajibu wa kila mmoja kutoa haki
katika kuzingatia sheria na kuepuka kuingilia majukumu ya mwingine bali waweze
kutekeleza majukumu yao katika nafasi zao kwa ajili ya maendeleo ya wilaya ya
Hai na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wa Wilaya
ya Hai na Siha Anold John Kirekiano amesema katika kutoa haki mahakama
inashirikiana na polisi,magereza pamoja na mihimili mingine ikiwa lengo ni kuhakikisha
nchi inasonga mbele kwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili.
Pia ameongeza kwa kusema kwamba kama mfumo wa
tehama ukitumika kikamilifu utaweza kurahisisha utendaji wa kazi na pia tehama
inanafasi zaidi kuhifadhi nyaraka
mbalimbali na ni salama.
No comments:
Post a Comment