Na Bahati Chume SIHA
Mgombea ubunge kupitia chama cha wananchi Cuf Tumsifieli Mwanry amesema akichaguliwa atahakikisha Wazee wanapata matibabu bila usumbufu wowote.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za ubunge kata ya ngarenairobi wilayani Siha, ambapo alisema ataandaa bajeti kwa ajili ya Wazee ili waweze kupata matibabu bila usumbufu wowote.
"wazee wamekuwa wakifika hospitalini wakiwa na vitambulisho lakini wanaambiwa wakanunue dawa kwamba zimekwisha"amesema Tumsifieli.
Ameongeza kwakusema "Mzee hana hela ndiyo maana amepewa kitambulisho lakini anaambiwa akanunue dawa ,nichagueni niweke bajeti kwa ajili ya matibabu ya Wazee" amesema Tumsifieli.
1 comment:
good
Post a Comment