Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania amekutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako Ikulu jijini Dar es
salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya
michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza
mawaziri hao kusimamia hilo.
Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment