Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 17, 2018 amepiga
marufuku aina yoyote ya michango katika shule za Serikali za msingi na
Sekondari nchini.
Raisi Magufuli amepiga
marufuku hiyo hiyo leo alipokutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam na
kuwataka mawaziri hao kwenda kusimamia jambo hilo na kuhakikisha hakuna michango
yoyote wanafunzi au wazazi wanachangishwa kwenye shule za sekondari.
Nae Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema
kuwa baadhi ya walimu ambao wamekuwa wakichukua michango ya wazazi na wanafunzi
na kuzipeleka kwenye mambo yao binafsi watashughulikiwa.
Waziri Jafo amesisitiza
kuwa hatua kali zitaanza kuchukuliwa ndani ya wiki hii na kuwataka wakuu wa
mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha mpaka siku ya Ijumaa wawe wamefikisha
taarifa za shule ambazo zilifanya jambo hilo na kukiuka utaratibu wa Serikali.
Waziri ndalichako ameagiza waalimu na viongozi wa halmashauri kuwarudishu shuleni mara moja wanafunzi wote waliorudishwa nyumbani kwakutotoa michango na pia kurejesha mara moja michango iliyokusanywa kinyume na muongozo wa serikali.
No comments:
Post a Comment