Na Praygod Munisi
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 23, 2018 ametengua
uteuzi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Butiama mkoani Mara Solomoni Ngiliule
kuanzia leo kutokana na ubadhirifu wa fedha za Umma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais TAMISEMI, Selemani Jafo ametangaza maamuzi hayo leo zikiwa zimepita siku
tatu toka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotoa maagizo kwa Kaimu Katibu Tawala
wa Mkoa wa Mara Bw. Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya
ukaguzi maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.
Waziri Mkuu aliagiza
kiongozi huyo kuchunguzwa kutokana na matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi
ya maendeleo zinazotolewa na Serikali zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia
kuandaa profile ya Halmashauri hiyo huku fedha zingine ni pamoja na sh. milioni
70 za elimu maalumu, sh. milioni 288 za mradi wa maji Butiama ambazo zote
hazikujulikani zimetumikaje.
No comments:
Post a Comment