Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa mkuu
wa Mkoa wa Kagera kufuatia vifo vya watu 11 waliofariki leo kwenye ajali
ya gari.
Kwenye
taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Serikali ambayo imeelezea jinsi Rais
alivyoguswa na kusikitishwa na vifo hivyo, na kuwafariji wafiwa katika
kipindi hiki kigumu.
"Nimehuzunishwa na kusikitishwa sana na vifo hivi, nawapa pole wafiwa wote na nawaombea marehemu wapumzike mahali pema, na majeruhi wapone haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku", imeandika taarifa hiyo.
Isome hapa taarifa yote

No comments:
Post a Comment