Na Praygod Munisi
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu ameeleza kuhusu hali yake ya kiafya inavyoendelea mpaka sasa huko nchini Kenya.
Akiongea na waandishi wa habari katika Hospitali ya Nairobi ambapo alikuwa anapatiwa matibabu, amesema, Madaktari wamefanikiwa kutoa risasi saba kati ya nane ambazo zilibakia katika mwili wake ambapo hiyo moja imeshindikana kutokana na sehemu iliyokuwepo inaweza ikaleta madhara makubwa endapo itatolewa.
“Madaktari wa Dodoma pamoja na madaktari wa Nairobi Hospital wametoa
risasi saba kuna moja bado haijatolewana wataalamu wamesema mahali ilipo
haina madhara kutakuwa na madhara zaidi wakijaribu kuitoa,” amesema
Lissu.
Mhe Lissu ameongeza kuwa katika tukio hilo la kushambuliwa lililomtokea Septemba 7 mwaka jana, alifyatuliwa takribani risasi 38 na kati ya hizo 16 zilifanikiwa kumpata na hizo nane ndio zilikwama katika mwili wake.
Kiongozi huyo alipelekwa katika hospitali hiyo ya Nairobi Septemba 8, 2017 ambapo ni takribani miezi minne mpaka sasa yupo nchini humo akipatiwa matibabu. Kwa sasa Lissu anapelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

No comments:
Post a Comment