Friday, 5 January 2018

DC HAI ATOA WITO KWA WAKUU WA SHULE



Na Elisha Eliakimu -HAI

Mkuu wa Wilaya ya Hai mshikizi, Onesmo Buswelu amewataka wakuu katika shule za sekondari  na waalimu wakuu katika shule za msingi kuakikisha wanafunzi wote  walioandikishwa  na waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaudhuria  shuleni pindi  shule  zitakapofunguliwa ili waweze kuanza masomo  yao.


Ameyasema hayo  leo  katika kikao  kilichowakutanisha maafisa elimu wa kata pamoja na  waalimu wa shule za msingi na sokondari  wilaya ya Hai, kwa lengo  la kujiandaa kufanya maandalizi ya kuuanza mwaka kitaaluma  kwa waalimu  kwa kipindi hiki cha kufungua shule.

Aidha Buswelu pia amewataka  makamu wa shule  zote za msingi na sekondari  kusaidiana  na wakuu wa shule katika usimamizi ili kuakikisha wanafunzi wanakuwa na nidhamu mashuleni na hata  majumbani.

Kwa upande wake afisa elimu  wa shule  za sekondari Halmashauri ya wilaya ya Hai Bw. Julius Kakyama  amewataka  waalimu  wakuu kuhakikisha  kuwa siku ya kufungua  shule  wanafunzi wote wanaingia darasani kwa ajili  ya kuanza masomo yao badala ya kufanya siku hiyo kuwa siku ya kufanya usafi mashuleni.

‘’kwa sababu tunaanza mwaka ni vizuri zaidi tukajipanga kwa pamoja tunaanzaje,je wanafunzi wanapokwenda kufungua shule tarehe nane jumatatu mwezi wa kwanza 2018,wanaanzaje na tukizingatia kwamba siku yakwanza yakufungua shule ni siku yakuingia darasani na jumla ya siku kwa mwaka za masomo ni 195,na siku zote lazima wanafunzi waingie darasani,kwa hiyo siku ya kwanza nilazima watoto waingie darasani”amesema Kakyama.

Ameongeza na kusemaa kuwa shule za sekondari zina uhaba wa waalimu wa sayansi na hisabati, huku idadi ya waalimu wa sanaa wakiwa ni wengi hivyo kupelekea kufanya mpango wa kuchukua waalimu wa sanaa katika shule za sekondari kwaajili ya kufundisha shule za msingi, na kwasasa wanasuburi mwongozo kutoka taifa ili waseme ni mbinu gani ambazo watatumia.

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...